24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Mamazulu Foundation yajitoa kuokoa kaya masikini na walemavu

Na Anne Ruhasha, Sengerema.

TAASISI isiyo  ya kiserikali ya Mamazulu Foundation ya nchini Uholanzi, imeendelea kujitoa kuokoa maisha ya watu wanaoishi kwenye Kaya masikini na watoto wenye ulemavu wilayani Sengerema mkoani Mwanza kwa kuwapatia misaada ya malazi.

Taarifa za taasisi hiyo zimeeleza kuwa tangu mwaka 2019 imeweza kusaidia kaya 20 zenye umasikini pamoja na kuendelea kutoa misaada kwa watoto wenye ulemavu kutoka shule mbalimbali za msingi wilayani humo.

Hadi sasa jumla ya watoto wenye ulemavu 158 ikiwamo wanafunzi 46 wa shule ya msingi Kizungwangoma, Busisi wanafunzi 56 na Chifunfu wanafunzi 56 huku taasisi hiyo ikitoa shilingi milioni 3.6 kwa mwaka kwa ajili ya chakula.

Mwenyekiti wa Mamazulu Foundation, Willeke de Mos akizungumza  katika moja ya familia aliyoipatia msaada amesema kwa miaka saba  imekuwa ikitoa misaada mbali mbali  kwa jamii hususani chakula kwenye shule za vitengo maalimu, ikiwamo Busisi, Kizingwangoma na Chifunfu, usafiri wa gari , bima za afya , sale za shule kwa watoto wenye uhitaji.

Willeke amesema toka amefika nchini amefanikiwa kutembelea baadhi ya familia zenye watoto walemavu waliopo chini ya ufadhili wake  na kupokea changamoto na baadhi alizitatua.

Ametaja mfano alitoa fedha za matibabu, viatu kwa watoto walemavu, na ununuzi wa magodoro kwa baadhi ya familia alizotembelea na kukuta watoto hao hawalalii magodoro.

Mmoja wa wanufaika wa misaada ya  MamaZulu Foundation, Bibi Chebelo ( 78) mkazi wa  kijiweni, kata ya Chifunfu anaeishi na wajukuu zake watano katika mazingira magumu ametoa chozi la furaha baada ya kununuliwa godoro na kusema tangu azaliwe  hajawai kulalia godoro.

Amesema kuwa mama wa watoto hao alifariki miaka mitano  iliyopita  ambaye alikuwa mtoto wake  huku baba watoto hao aliwakimbia kutokana na mmoja wao kuwa mlemavu wa akili na yeye kama bibi.

Licha ya kuwa na umri mkubwa amesema anajishughulisha na kuokota dagaa katika mwalo wa kijiweni kwa lengo la kujipatia kipato na chakula cha wajukuu zake .

Ameeleza kuwa mwaka 2019  Mamazulu foundation walifika nyumbani  kwake  kwa lengo la kumsaidia mjukuu wake mlemavu kumpeleke shule na kumpatia chakula  ambapo msaada huo umesaidia familia nzima na kufungua milango ya mafanikio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles