25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 7, 2024

Contact us: [email protected]

Mama Lui yawakumbuka watoto Mwanza maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KATIKA kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika leo Desemba 9, Mwekezaji wa maduka ya watoto, Louis Bonzon, amefungua rasmi duka la vifaa vya watoto jijini Mwanza litakalowasaidia kupata vifaa vya kuwasaidia kupanua upeo wa akili na kucheza.

Duka hilo ambalo limefunguliwa leo rasmi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mbugani jijini hapa, litakuwa maalum kwa vifaa vya watoto kwa ajili ya sherehe za watoto, muziki, mabembea, vishikwambi, vifaa vya muziki, michezo (games), michezo ya mafumbo (cube, puzzle blocks) na vingine vingi.

Akizungumzia dhima ya kufungua duka hilo, Bonzon, amesema duka hilo lenye makao yake makuu mjini Moshi baada ya kufanya tathmini walibaini kwamba Manza kuna fursa kwani hakuna vitu vingi vya kuwasaidia watoto kucheza na kujifunza, hivyo wakaamua kuja na biashara hiyo ambayo kwa sasa watauza kwa rejareja na bei nafuu lakini kuanzia Januari, mwakani wataanza kuuza na kwa wateja wa jumla.

“Leo tukisherehekea miaka 62 ya Uhuru wa taifa letu tumeona ni siku nzuri kufungua duka letu hapa tunawakumbuka watoto ambao ni kama walisahaulika hawakuwa na sehemu maalum inayopatikana bidhaa zao, kwahiyo tuliona fursa hiyo ya vitu vya watoto kujifunza na kupanua upeo wa akili,” amesema na kuongeza;

“Wazazi wamekuwa wakiona ni gharama kufanya matumizi kwa ajili ya watoto kwahiyo tukiwa na vitu vizuri na bei ya chini tutawavutia. Napenda kushauri watu wasiishi kwenye mazingira ya kuigana wanapoanzisha biashara bali wafikirie kwanza kitu ambacho kwenye mazingira aliyopo hakipo ili ajihakikishie wateja na kuendeleza biashara yako,” amesema.

Mmoja wa wazazi ambao wamefika na kununua bidhaa, Salama Nduta mkazi wa Bukoba ambaye amekuja kwenye sherehe ya mtoto wake anayesoma chekechea, amesema;

“Nimepita hapa kununua keki ni nzuri na zina bei nzuri nimefurahishwa na bidhaa na bei zao, pia sisi tunaojishughulisha na mapambo wana vitu vingi vinavyotusaidia kwenye kazi yetu,”.

Akizungumza baada ya kuzindua duka hilo, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mbugani, Mwanza, Werema Masero, amesema uwepo wa duka hilo katika kata yao umetia hamasa na kukuza uchumi wa eneo hilo huku akiwasihi wajasiriamali wasiogope kufungua biashara katika kata hiyo kwani mkoa wa Mwanza una fursa nyingi za uwekezaji.

“Tumefarijika kuona wajasiriamali wanakuwa wabunifu na kusaidia jamii kupiga hatua hii inaleta hamasa kwa Watanzania wengine,” amesema.

Naye, Diwani wa Kata ya Mbugani, Ezekiel Emmanuel, amesema “Uwepo wa duka hili unaleta mvuto katika kata yetu, wananchi wangu wamekuwa wakienda kwenye maduka katika maeneo mengine huyu ametufungulia njia inatupa ujasiri wa kushawishi watu wengine kuwekeza hapa kwetu. Tuendelee kushirikiana na wajasiriamali kama hawa kwa kuwaunga mkono kuhakikisha wanapiga hatua,”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles