Mama awataka Blac na Rob waoane

0
591

Rob na BlacLOA ANGELES, MAREKANI

MAMA wa Blac Chyna, Shalana Hunter, amemtaka mwanawe kuoana na mpenzi wake, Rob Kardashian.

Wawili hao wameanzisha uhusiano mwanzoni mwa mwaka huu, lakini uhusiano wao umekuwa na utata katika familia ya Kardashian kutokana na Blac kutoka na msanii wa hip hop, Tyga ambaye kwa sasa msanii huyo anatoka na mdogo wa Kim Kardashian, Kylie Janner.

Kutokana na hali hiyo, familia ya Kardashian ilifikia hatua ya kugombana na ndugu yao, Rob kutokana na msichana huyo, lakini mama wa Blac amewataka wawili hao kuoana.

“Ni vizuri mipango ya ndoa ikaanza kufanyika mapema iwezekanavyo ili kuweza kupunguza maneno ya watu ambayo yanaendelea kwenye mitandao ya kijamii,” alisema mama wa Blac.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here