Justin Bieber asokota rasta

0
910

BeiberNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki wa Pop nchini Marekani, Justin Bieber, amewashangaza watu baada ya kupanda jukwaani kwenye tuzo za muziki za HeartRadio huku nywele zake zikiwa zimesokotwa rasta.

Msanii huyo alikuwa akivaa kofia mara kwa mara kwa ajili ya kuzificha nywele hizo, lakini juzi aliamua kuziweka wazi kwa mashabiki wake.

Katika tuzo hizo, Bieber alifanikiwa kuondoka na tuzo ya msanii bora wa kiume wa mwaka jana na wimbo wa mwaka wa ‘Where Are U Now’.

Hata hivyo, msanii huyo kupitia akaunti yake ya Instagram, aliweka picha yake na kuwataka mashabiki wake washishangae mwonekano wake mpya wa sasa.

“Najua watu wengi wameshangaa kuona nikiwa na rasta, lakini huu ni mwonekano wangu mpya hivyo mashabiki wasishangae kwa kuwa ni moja ya aina ya maisha yangu,” aliandika Bieber.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here