25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MAMA AMWANDAA BINTIYE KUTWAA TAJI LA UREMBO WA DUNIA

KWA wazazi wengi wenye kufahamu wajibu wao kitu cha kwanza hupenda kuwekeza kwa watoto wao wadogo ni elimu na makuzi katika maadili ili kuwaandaliz mazingira mazuri kwa miaka yao ya badaye.

Lakini kwa mama huyo dogo nchini Uingereza, hilo amelichukulia kwa namna tofauti, ambayo ana amini ni sahihi kwa mwelekeo wa baadaye wa bintiye.

Enrika Milne (26), ametumia maelfu ya pauni za Uingereza kumtengeneza bintiye mdogo  vipodozi, kucha na nywele bandia kwa kile anachodai kumjengea mazingira mazuri ya baadaye.

Hatua zake hizo zimemfanya akumbane na shutuma kutoka kila kona katika mitandao ya jamii, ikimkosoa kuwa anamharibu malkia wake dogo wa urembo mwenye umri wa miaka minne.

Mkazi huyo wa Sheppey, Kent hutumia saa mbili hadi tatu kumwandaa bintiye huyo Arielle (4) kwa mashindano ya urembo, akidai anamfundisha na kumwandaa kuwa Miss England ajaye atakayetikisa Miss World (taji la Urembo wa Dunia).

Mama huyo alisema: ‘Nitajisikia vibaya iwapo nitaacha kufanya ninachofanya sasa, kwa vile ni vitu vilivyomjenga bintiye kuwa mwenye kujiamini na nimemfundisha kila kitu kuhusu shughuli za hisani.”

“Katika mashindano mengi ya urembo, washiriki huchangisha fedha kwa ajili ya shughuli za hisani pia hivyo ni muhimu kujifunza,” anasema.

Tangu aanze kushiriki mashindano ya urembo Aprili 2016, malkia huyo dogo wa urembo ametwaa dazeni ya mataji huku akiwateka mashabiki kwa mitindo ya mavazi yake.

Lakini Enrika, ambaye anatumia pauni 350 sawa na zaidi  Sh. 900,000 kumwandaa Arielle kwa shindano moja la urembo, analazimika kujitetea dhidi ya shutuma kuwa anamharibu bintiye kumtengeneza kwa namna inayotamanisha kingono.

Anaendelea: ‘sisi (tasnia ya urembo) ni kawaida kuchukuliwa vibaya, lakini nataka Arielle afanye kile kinamchomfanya awe na furaha,’ alisema.

Mashindano ya urembo yamekuwa ya kustaajabisha na yamemuimarisha kwa kumfanya ajiamini. Watoto wengi wa umri wake wanapata tabu kujieleza na kujiamini, lakini binti yangu hana tatizo hilo. Tayari ana jiamini katika umri wa miaka minne tu, hakika anatarajia kuja kufanya mambo makubwa siku za usoni.

‘Namtaka awe Miss England siku moja na nadhani kujikita katika urembo kutaendelea kumfanya katika njia nzuri na kuzuia asipotoke kwa kujiingiza katika matumizi ya ulevi na uvutaji katika miaka yake ya ujana.

Enrika, ambaye anaendesha biashara ya urembo na ambaye ameolewa na Mkurugenzi wa kampuni Wayne (35), aliangukia katika mashindano ya urembo tangu ayaone katika televisheni.

Wakati Arielle akiwa mdogo wakati huo, Enrika alisubiri kwa miaka michache kabla ya kutamba katika Facebook akishiriki mashindano yanayofanyika mji wake wa nyumbani.

Kisha Aprili 2016, dogo huyo akaingia jukwaani kwa mara ya kwanza, ambapo aliweza kuteka hadhila na kuwa kipenzi cha wengi.

Enrika aliongeza: kamwe sikutaka kumfanya Arielle afanye kitu fulani lakini kwanza alihitaji kutiwa mioyo.’

Sasa, Enrika na Arielle wamesafiri kote nchini Uingereza huku Wayne akiwa dereva wao wakishiriki shindano moja baada ya lingine na hata kumsaidia bintiye kuwa tayari kwa kusaidia nywele na kumpaka rangi.

Akitumia utaalamu wake wa urembo Enrika humremba Arielle mwenyewe kwa vipodozi, akimwingiza nyusi, rangi ya mdomo na kadhalika.

Dogo huyo pia huvaa nywele zenye thamani ya pauni 100 sawa na Sh 300,000 na kucha maalumu bandia anazorembwa na mama yake.

‘Katika maisha ya kila siku, huvaa nywele bandia na kupaka kucha, ambayo humfanyia kila wiki,’ aliongeza Enrika.

“Hatumii vipodozi kila siku lakini anaweza kujitengeneza mwenyewe. Anafanya vyema, anaweza kujipamba nyusi.

“Huwa hapendelei nyusi bandia, lakini huzivaa wakati wa mashindano.”

Kwa gharama za vipodozi kwa Arielle– ambavyo vinaweza kugharimu pauni 300 sawa na zaidi Sh 900,000 kwa wakati mmoja– kusafiri na kukaa hotelini wakati wa kushiriki mashindano mbali na nyumbani, Enrika anakadiria kwamba ametapanya maelfu ya pauni kwa ajili ya ‘hobby’ hiyo.

Anaendelea: ‘Ina thamani ya kila senti, wakati unavyoona namna Arielle alivyo jiamini. Anashangaza kwa umri wake na huweza kutengeneza blogu ya video kuhusu maisha yake.

“Naona mashindano ya urembo ni kama uwekezaji wa wakati ujao. Yana gharama lakini unahitaji kuwa maalumu ili kuwavutia majaji.”

Enrika alisema kuwa yeye na Wayne hupendelea kushiriki kikamilifu katika majukwaa ya mashindano ya urembo, kwa vile pia huwawezesha kufurahia wakati bora wa kifamilia.

Aliendelea: ‘tunaweza wakati mwingine kuwa nje ya nyumbani kwa wiki tatu kwa mwezi, hivyo, naipenda kwa sababu Wayne pia huja pamoja nasi.

‘Ni nadra kuwaona kina baba katika mashindano ya urembo. Kila mtu humpenda, ni mwingi wa utani na hakika husaidia.

“Ana msaada mkubwa. Hujifunza pia namna ya kumpaka Arielle vipodozi vya rangi alivyojifunza kwa kuniangalia.

Wayne alisema: ‘Ninajihusisha sana na tasinia hii. Nasaidia kila inapobidi kama vile kupaka rangi, kutengeneza nywele na kupaka vipodozi vingine.

“Kina mama wengine huniita baba wa mashindano ya urembo wa mwaka. Kuna kina wababa wachache wanaojishughulisha katika tasnia hii.

‘Wengi utawaona wamebana kona kana kwamba hawana habari au kujificha siku nzima, lakini si mimi. Mara nyingi naonekana hadharani nikitoa maoni yangu na kina mama wengine.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles