29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

NJIWA AENDA JELA KWA KUMTISHIA WAZIRI MKUU

NEW DELHI, INDIA

NI ajabu na kweli na kwa wapenzi wafilamu watakuwa wamewahi  kuona filamu hasa zenye maudhui ya kale zikionesha namna watu walivyokuwa wakitumiana ujumbe kutoka umbali mrefu kupitia wanyama warukao yaani ndege.

Basi hivi karibuni polisi nchini India walimkamata njiwa aliyekuwa amebeba ujumbe akiwa ametumwa kuuleta humo kutoka Pakistan.

Njiwa huyo wa rangi ya kijivu aliyekuwa na ujumbe wenye vitisho uliomlenga Waziri Mkuu Narendra Modi alivuka mpaka wa nchi hiyo na Pakistan ambako kuna ulinzi mkali wa kijeshi.

Maafisa wa Kikosi cha Ulinzi wa Mpakani (BSF) walimkamata ndege huyo katika eneo la Pathankot, jimbo la kaskazini ya Punjab, ambako wanajeshi wa Pakistan walifanya shambulio lililosababisha maafa Januari mwaka huu.

“Tulimweka kizuizini jana jioni,” Inspekta wa Polisi wa Pathankot, Rakesh Kumar aliwaambia wanahabari kwa njia ya simu.

“BSF walimkuta akiwa na barua iliyoandikwa kwa lugha ya Urdu ikisema kitu kama, ‘Mordi, hatuko kama tuilivyokuwa mwaka 1971. Wakati huu kila mtoto yuko tayari kupigana dhidi ya India,” alisema Kumar.

 

Mataifa haya jirani, ambayo awali yalikuwa taifa moja yalipigana vita kali mara ya mwisho mwaka 1971.

Barua hiyo ilionekana kutiwa sahihi na kundi la wanamgambo la Lashkar-e-Taiba (LeT) lililo Pakistan.

“Tunachunguza jambo hilo kwani tumelichukulia kwa uzito mkubwa,” alisema Kumar.

Hii si mara ya kwanza kwa ndege kuhusishwa kwenye uhasama ulio kati ya nchi hizo mbili zenye silaha za kinyuklia.

Hivi majuzi walipatikana Punjab wakiwa na ujumbe kama huo kwa Mordi kwa lugha ya Urdu.

Mwaka 2015, polisi wa India walikamata njiwa aliyeshukiwa kutumiwa na Pakistan kufanya ujasusi, kisha wakamweka kwenye mitambo kumkagua kama kulikuwa na kamera ya siri au chombo chochote cha kidijitali cha kukusanya habari kisiri.

Katika mwaka wa 2013, polisi wa India walipata mzoga wa ndege aina ya kipanga aliyekuwa na kamera ndogo, na katika mwaka wa 2010, njiwa mwingine alikamatwa kwa madai ya kufanya ujasusi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles