24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Malaysia yamwacha huru mshukiwa wa mauaji

KUALA LUMPUR, MALAYSIA

MAHAKAMA nchini Malaysia imemwachia huru, Doan Thi Huong, ambaye ni raia wa Vietnam aliyekuwa akituhumiwa kwa mauaji ya ndugu ya baba mmoja wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, baada ya waendesha mashtaka kuiondosha kesi hiyo.

Doan Thi Huong, mwenye umri wa miaka 30, alikuwa kizuizini mwa muda wa miaka miwili sambamba na mwanamke mwingine raia wa Indonesia, wakituhumiwa kumpaka sumu usoni, Kim Jong Nam, katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, Februari 2017.

Korea ya Kusini na Marekani zimekuwa zikisema kuwa mauaji hayo yaliratibiwa na majasusi wa Korea Kaskazini, huku mawakili wa utetezi wakisema wateja wao walitumiwa kama kichaka cha kuficha njama hiyo.

Waendesha mashtaka walifuta shtaka la mauaji mwezi uliopita, baada ya Huong kukubali kukiri shtaka jingine la kusababisha madhara. Wakili wake, Hisyam Teh, amesema mteja wake anatarajiwa kurudi kwao Vietnam baadaye leo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles