27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Siku ya Wakunga duniani kitaifa kufanyika Simiyu

Derick Milton, Simiyu

Maadhimisho ya Siku ya Wakunga duniani kitaifa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kesho Jumapili Mei 5, mkoani Simiyu, ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndungulile.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Mkuu wa mkoa wa huo, Anthony Mtaka, Naibu Waziri huyo atamwakilisha Makamu wa Rais wa Samia Suluhu Hassan.

Mtaka amesema kuwa maandalizi yote ya maadhimisho hayo yamekamilika kwa asilimia 100, ikiwamo wakunga kutoka katika mikoa mbalimbali wakiongozwa na viongozi wa chama chao (TAMA) kuwasili mkoani humo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAMA, Feddy Mwanga, amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni; ‘Wakunga watetezi wa haki za binadamu’.

“Katika maadhimisho haya, kama chama tunajivunia kushirikiana na serikali katika kuwajengea uwezo wakunga kutoa huduma ya dharura na iliyo bora kwa mjamzito anayepata tatizo la kutokwa damu nyingi wakati wa kujifungua,” amesema Mwanga.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Hashina Bergan, amesema ili kupunguza vifo vya wajawazito ni lazima kuboreshwa kwa mfumo wa uuguzi na ukunga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles