24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Makusanyo bandari ya Bukoba yaongezeka

ESTHER MBUSSI-BUKOBA

MFUMO wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kieletroniki, umesababisha ongezeko la makusanyo katika Bandari ya Bukoba mkoani Kagera, kutoka Sh milioni 21 hadi 29 hadi Sh milioni 60 hadi 69 kwa mwezi.

Kaimu Meneja wa Bandari za Kanda ya Ziwa, Geofrey Lwesya amewaambia waandishi wa habari bandarini hapo jana makusanyo hayo yanatokana na wafanyabiashara wakubwa wanaotumia bandari hiyo ikiwamo wanaotoa bidhaa Uganda na Kiwanda cha Sukari cha Kagera (Kagera Sugar) ambaye ndiye mteja mkubwa.

Aidha, amesema mapato hayo huenda yakaongezeka baada ya ujenzi wa meli kubwa ya abiria na mizigo unaotarajiwa kukamilika Septemba mwaka 2020.
Pamoja na ujenzi wa meli hiyo pia ujenzi wa gati la kisasa unaoweza kuhimili meli zote na boti.

“Baadhi ya majengo muhimu yakiwamo majengo ya abiria, sehemu za kuhifadhia mizigo, vyoo vya kisasa, vibanda vya walinzi na zote vyenye ubora wa kisasa yao katika hatua za mwisho ambapo tumeboresha maneo bandari yetu iendane na huduma zinazotolewa na bandari hiyo.

“Jengo la abiria la kisasa limekarabatiwa pamoja na ofisi ujenzi uliogharimu Sh milioni 143.8, kwa sababu tunatarajia Meli ya MV Victoria ambayo inafanyiwa marekebisho ya kubeba abiria na mizigo kuanzia tani 1,200 hadi 4,000.
“Pia kuna meli ndogo maalumu zinazohifadhi ubaridi kwa ajili ya kubebea samaki kutoka visiwani na kupelekwa viwandani,” alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Bandari hiyo, Bulenga Ndalo alisema meli ndiyo usafiri muhimu unaotegemewa Bukoba hivyo kusimama kwa huduma hiyo kumesababisha adha kwa watu wengi kwani kwa sasa bandari hiyo ambayo inahudumia visiwa viwili vya Kerebe na Gozba, haina meli ya abiria bali wanategemea boti kwa ajili ya usafiri.

“Zamani kulikuwa na meli mbili za mizigo lakini sasa kuna meli tano kubwa zinazoingia kwa mwezi mizigo mbalimbali ikiwamo vifaa vya dukani wa tani 200 mkubwa ukiingizwa na Kiwanda cha Kagera Sugar ambao ni tani 3,500,” alisema.

Alisema baada ya wadau na wafanyabiashara kusikia kuna ujenzi wa meli kubwa wamefarijika sana.

Akizungumzia huduma katika bandari hiyo, Nahodha wa Meli ya MV Luxury II, Peter Hiza, alisema anapata huduma nzuri ikiwamo kupakia na kushusha mzigo kwa wakati ambapo kwa wakati muafaka.
Alisema meli yake imeingia ubia na Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) kutoa na kupeleka Bukoba kutoka Mwanza.


“Tunatumia bandari za serikali kutokana na gharama za kawaida ambapo huwa nakuja kuleta mara mbili kwa mwezi kuleta mzigo,” alisema.

Shamsa Mohammed mwakilishi wa Kagera Sugar, alisema meli mpya kwa hamu kubwa kwani kuna unafuu mkubwa katika usafiri wa mjini kuliko barabara katika kusafirisha sukari.


“Tani tunazosafirisha kutoka Bukoba kwenda mikoa mingine tunatumia meli kwani ina gharama nafuu na inafika salama,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles