30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Kamati Kuu ACT yajadili ajenda mbili

ASHA BANI –DAR ES SALAAM 

KAMATI Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo, imekutana Dar es Salaam ikiwa na ajenda kuu mbili.

Ajenda hizo ni kampeni ya ‘Shusha tanga, pandisha tanga’ iliyofanikiwa kwa kuvuna wanachama kutoka sehemu mbalimbali na namna ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika baadae mwaka huu.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kiongozi Mkuu, Zitto Kabwe, mwanachama mwenye kadi namba moja, Maalim Seif Sharif Hamad na kada wa chama hicho, Juma Duni Haji.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi, Ado Shaibu, alisema wanajadili mafanikio ya mikutano yao ya pandisha tanga shusha tanga.

 “Kikao cha Kamati Kuu ndiyo cha kwanza na kinajadili mambo mbalimbali, yakiwamo pandisha tanga, shusha tanga na jinsi ilivyofanikiwa kupokea wanachama wengi mashuhuri, sambamba na wanachama wengine zaidi ya 80 waliojiunga na chama chetu.

“Tunaangalia jinsi ambavyo ACT-Wazalendo kwa upande wa Bara ilivyoleta mageuzi na kutafakari mambo mbalimbali ya kisiasa ya ndani na siasa za jumla na kisha kutoa majumuisho baadaye,” alisema Shaibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles