25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda amtaka mratibu Tarura kupiga kambi Tamisemi

Brighiter Masaki – Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtaka Mratibu wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura)  mkoani humo, George Tarimo kwenda kupiga kambi ofisi za Tamisemi hadi atakapopata majibu ya malipo ya fidia ya fedha za ujenzi wa barabara ya wakazi wa Makongo.

Alisema zaidi ya Sh bilioni 4 zinapaswa kulipwa fidia ili kupisha ujenzi wa barabara inayoanzia Chuo cha Ardhi, Makongo hadi Goba.

Akizungumza jana Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Bodi ya Barabara ambao ulihusisha kamati tano ambazo zilienda kufanya tathmini na kuleta changamoto na ushauri nini kifanyike ili kuweza kufanya ukarabati wa barabara hizo.

Makonda alipokea tathmini ya hali ya barabara ya Wilaya ya Kinondoni, ambapo alimtaka mratibu wa Tarura kuanzia leo asifike ofisini isipokuwa aende Tamisemi akatafute majibu ya fidia hiyo.

“Kesho ondoka nisikuone mkoani mpaka utakapokuja na pesa za Makongo, mnakaa kusubiri majibu labda hawajaona barua, kaweke kambi mpaka upate hela,” alisema Makonda.

Awali Tarimo alisema bado hawajapewa majibu ya malipo ya fidia hiyo licha ya kuwa waliwasilisha maombi.

“Fidia tuliwasilisha hatujapata majibu,” alijibu Tarimo.

Akiwasilisha taarifa ya hali ya barabara za Wilaya ya Kinondoni, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia (CCM), alisema ili mkandarasi aendelee na ujenzi wa barabara hiyo lazima fidia ilipwe.

Alisema ujenzi wa barabara hiyo unagharimu Sh bilioni 8.2.

Kutokana na hali hiyo, Makonda ameagiza fedha zote Sh bilioni 165 zilizotengwa kwa ukarabati wa barabara za mkoa huo katika bajeti ya 2019/20 zitumike kama zilivyopangwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles