23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Makete yaanza kampeni kilimo cha parachichi

NA MWANDISHI WETU, Mtanzania Digital

TAASISI na Vikundi kutoka Kata mbalimbali wilayani Makete, wamegaiwa miche zaidi ya 5000 ya parachichi ili kuongeza chachu ya uzalishaji na kulima zao hilo.

Kampeni hiyo inatokana na parachichi kupatizwa jina la dhahabu ya kijani mkoani Njombe ambapo tayari Serikali imeanza kugawa miche ya zao hilo bure kwenye Taasisi za shule na vikundi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi miche hiyo katika Kata ya Matamba wilayani humo,Mbunge Jimbo la Makete, Festo Sanga amesema wataanza kampeni ya Wilaya nzima kwa kila Kaya kuwa na miti 50 ya parachichi.

“Serikali imeanza zoezi hili muhimu kwa wananchi ambapo tutakuja na Kampeni kwa Wilaya nzima ya Makete kila Kaya kuwa na miti 50 ya parachichi,” amesema Sanga.

Kwa upande wake Ofisa Kilimo Wilaya ya Makete, Aniseti Ndunguru, amesema Serikali imepanga kuanzisha uzalishaji kwenye vitalu vya zao hilo ili kurahisisha upatikanaji wa miche ndani ya Wilaya hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles