27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

Makalla awataka wahalifu kujisalimisha mikononi mwa Polisi

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuhakikisha linawashughulikia kikamilifu Majambazi na Vibaka Jijini humo huku akiwataka kujisalimisha na kukabidhi Silaha zao kwa hiyari.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo, ofisini kwake, Makalla ameagiza kuanza kwa Operesheni ya kufagia watu wote wanaofanya Vitendo vya uhalifu Jijini humo.

Amesema ni vyema pia wazazi wakaanza kuwaonya watoto wao pindi wanapoona Wana mienendo isiyoeleweka.

Makalla amesema kwakuwa uzoefu unaonyesha wahalifu hao hutumia Silaha kujerui na kusababisha vifo, ni vyema Jeshi la Polisi likawawahi kuwashughulikia kikamilifu Majambazi kabla hawajatumia Silaha hizo kujerui na kusababisha vifo kwa Wananchi.

Aidha Makalla, amewahikikishia Wananchi wa mkoa huo Usalama na kuwataka kuendelea na majukumu yao kama kawaida kwakuwa vyombo vya Ulinzi na usalama vimejidhatiti kulinda usalama wa raia na mali zao.

“Wananchi wa Dar es Salaam, mpo salama Jeshi la polisi lina walinda ninyi na mali zenu,” amesema Makalla

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Camilius Wambura amesema Katika msako ulioanza Mei 21 hadi 25 wamefanikiwa kuwakamata Majambazi na Vitu mbalimbali ikiwemo magari Manne, Pikipiki moja, Bunduki Moja, Laptop na vifaa vinginevyo.

Aidha Kamanda Wambura, amemuhakikishia Makalla, kuwa maagizo aliyoyatoa wameyapokea kwa mikono miwili na watayafanyia kazi kwa ufanisi mkubwa.

“Wanaofanya uhalifu wakae wakijuwa, Dar es Salaam na Tanzania sio salama kwao katika kazi zao za uhalifu wanazozifanya,” amesema Wambura.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,414FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles