22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Polisi Dar yadaka watuhumiwa 20 wa ujambazi

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam katika kupambana na vitendo vya kihalifu limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 20 kwa vitendo vya uhalifu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Mei 25, 2921 jijini Dar es Salaam, Kamanda Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Camillius Wambura, amesema kuwa Jeshi lipo imara na limejipanga vizuri kuhakikisha hali ya Jiji inaendelea kuwa shwari

Amesema Machi 18, 2021 saa 8.00 usiku tumefanikiwa kuwakamata majambazi watano.

“Majambazi hao walivamia katika nyumba ya Mkurugenzi wa Benki ya Azania iliyopo Mbweni Mpiji na kuwashambulia walinzi wa kampuni ya SUMA JKT na kuwapora silaha aina ya Short Gun Pump Action ikiwa na risasi tano,” amesema Wambura.

Amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum lilifatilia na kufanikiwa kukamata silaha hiyo Mei 20, 2021 na watuhumiwa watano waliohusika katika tukio hilo.

“Jeshi la polisi linawashikilia watu watano kwa tuhuma za mauaji, ambao ni Issa Karim maarufu kama ‘Mdaka Bomu'(33), Mohamed Juma(31), Selemani Seif maarufu kama ‘Dullah Kishandu'(34), Samsoni Joseph maarufu kama ‘Mjeuri’ (32) na Ezekiel Kenned maarufu ‘Simba MC’ wote wakazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam.

“Mei 8, 2021 saa 8:05 usiku Mikocheni A watuhumiwa hawa walivamia katika Baa iitwayo Imbizo Bar na kumshambulia kwa mapanga na marungu mlinzi aliyefahamika kwa jina, Regan Sylivester na kusababisha kufariki dunia papo hapo.

“Watuhumiwa wanahusika na tukio la unyan’ganyi wa kutumia silaha huko Mabwepande ambapo mnamo tarehe 07/05/2021 saa 9:00 usiku walivamia katika kituo cha kuuzia Mafuta (Petrol Station) cha MEXONS na kuwashambulia walinzi, wahudumu na wateja na kupora kiasi cha Tsh 2, 440,000/= na kisha kupora silaha aina ya Short Gun ya walinzi hao,” amesema

Wakati huo huo
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata magari manne na watuhumiwa wanne.

“Watuhumiwa tuliokamatwa ni Babuelly Simon Chao, Miaka 43, mkazi wa Moshi, Sebastiani Shembaru, Miaka 36, mkazi wa Kigamboni, Hussen Misanya, miaka 33, Mkazi Mabibo Relini na Said Rajabu, miaka 16, mkazi wa Mabibo,” amesema Kamanda.

Aidha ameongeza kuwa watuhumiwa hawa wamekuwa wakiiba magari maeneo ya Kinondoni na Ilala na walikamatwa na magari yenye namba
T 817 ATQ Toyota Nadia, T 134 BPJ Toyota IST, T 952 CKB Toyota Mark II Grand, T 590 DTK Toyota IST.

“Tumefanikiwa kukamata Pikipiki namba MC 136 CSA Boxer nyeusi iliyokwa imeibiwa Mei 15, 2021 huko maeneo ya Kibamba shule na kupelekwa Gairo Mkoani Morogoro.

“Jeshi la Polisi Kanda lilifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kuikamata pikipiki hiyo na kuirudisha Jijini DSM,” amesema Wambura.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles