24.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali yaanza utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia, IMF

Na Farida Ramadhan, WFM – Dodoma

Serikali imeanza utekelezaji wa maelekezo ya kikao cha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Kimataifa (IMF), Kristalina Georgieva kilichofanyika kwa njia ya mtandao mwanzoni mwa mwezi huu ambacho pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu atheri za kiuchumu na kijamii zilizotokana na changamoto za janga korona (Covid- 19).

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza wakati wa kikao na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kilichofanyika jijini Dodoma.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa IMF nchini, Jens Reinke katika ofisi za Wizara hiyo.

Amesema wamekutana ili kutafsiri maelekezo hayo katika utekelezaji ili kuiwezesha IMF kushirikiana na Tanzania katika kujenga uchumi ambao umekumbana na misukosuko inayoendelea duniani inayotokana na changamoto za janga la korona (Covid- 19).

Tumekutana na IMF pamoja na Wataalam wa Wizara pamoja na baadhi ya taasisi zake kujadili namna ya kuandaa taarifa ya maeneo yaliyoathirika zaidi na misukosuko hiyo pamoja na kuangalia kiwango cha athari katika maeneo husika,” amesema Dk. Nchemba.

Dk. Nchemba alisema athari za misukosuko hiyo ya uchumi zinatofautiana kisekta kwa kuwa kuna sekta ambazo zimeathirika moja kwa moja kama biashara, utalii na makusanyo, na kuna zile ambazo haziathiriki moja kwa moja.

Alisema wataangalia athari za misukusuko hiyo katika huduma za jamii kwa upana wake kama huduma za Afya hususani kuboresha miundombinu, dawa na upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na suala la upatikanaji wa maji.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa IMF nchini, Jens Reinke alisema shirika hilo lipo tayari kushirikiana na Tanzania na kubainisha kuwa yeye binafsi yupo tayari kufanya kazi na wataalam wa Tanzania ili kusaidia nchi na kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa kwa kasi kama ilivyopangwa.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayeshughulikia Maendeleo na Biashara Afrika Mashariki, Bi. Nnenna Nwabufo kuhusu namna bora ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na benki hiyo.

Dk. Nchemba alisema Serikali itaufanyia kazi ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na benki hiyo ili kuhakikisha kuwa miradi yote inayofadhiliwa inatekelezwa kwa haraka kama ilivyopangwa.

“Benki ya Maendeleo ya Afrika ni miongoni mwa benki ambazo zinatoa fedha nyingi katika hudumia miradi nchini hususan miradi ya miundombinu, na kesho Mwakilishi wa Benki na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha watasaini mkataba kule Dar es Salaam kwa ajili ya miradi,” amebainisha Dk. Nchemba.

Alisema kwasasa benki hiyo inafadhili miradi ya miundombinu takribani 22 ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko mkoani Dodoma na mradi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato jijini Dodoma.

Afafanua kuwa Serikali inangojea utekelezaji wa benki hiyo kuwezesha Tanzania kunufaika zaidi na madirisha ya mikopo inayotolewa ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayeshughulikia Maendeleo na Biashara Afrika Mashariki, Nnenna Nwabufo alisema benki hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali.

Alisema benki hiyo iko tayari kuyafanyia kazi mambo yote muhimu waliyojadili ikiwa ni pamoja na kuwezesha Tanzania kunufaika zaidi na madirisha ya mikopo inayotolewa.

Aidha, Nwabufo alimpongenza Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kupata nafasi hiyo na kutoa salam za pole kutokana na msiba mzito ulioikumba nchi kwa kuondokewa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Pombe Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,264FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles