23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Makalla agiza ombaomba kuondoka Dar es salaam

Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amewaagiza wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri za Dar es Salaam kuratibu zoezi la kuondoa ombaomba na kuwarudisha makwao.

Amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona kwa kuvaa barakoa.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati akifungua mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kuweka mikakati kuhusu ukatili wa watoto.

Amesema tatizo la ombaomba limekuwa sugu kwa Dar es Salaam na linachangiwa na baadhi ya watu ambao wanawaleta watu kutoka mikoani na kuwafanya mradi.

“Mimi nasema hatukubali kuona mawakala wa ombaomba wanaendelea kuwaleta, wachague kazi nyingine. Yaani mtu anafanya mradi anatuona sisi wajinga. Wakuu wa wilaya, wakurugenzi tuanze na hao, tuwabaini na hatua zichukuliwe,” amesema.

Amefafanua kuwa, ofisi ya mkoa itatoa mabasi ya kuwarudisha makwao hivyo kuanzia Juni, waanze kuandikisha majina yao.

“Waandikishe majina yao tena kwa hiari yao wenyewe, na wataondoka. Kwa hiyo ombaomba wanaotaka kurudi kwao ofisi ya mkoa ipo tayari na iratibu jambo hili,” amesema.

Kuhusu kuchukua tahadhari ya maambuzi ya virusi vya corona, amesema jambo la msingi katika kufanya kila kitu ni afya, hivyo wasione aibu kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa.

“Huwezi kufanya biashara kama huna afya njema. Tahadhari ni jambo la muhimu sana na msione aibu wala usifikiri mtu ambaye hajavaa barakoa atakuelewa vibaya, mdau wa afya yako ni wewe mwenyewe. Kwa hiyo tusioneane aibu, tuchukue tahadhari kwani haina gharama yoyote unapovaa barakoa. Lakini ukichukua tahadhari kazi iendelee,” amesema.

Pia ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushughulikia wale wote ambao wanawalaghai wanafunzi na kufanya nao ngono.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles