31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa dini Kilimanjaro walia na kukithiri kwa rushwa, unyaji pombe

Na Upendo Mosha,Moshi

Viongozi mbalimbali wa dini mkoani Kilimanjaro wametoa malalamiko kwa Serikali ya mkoa huo ya kukithiri kwa vitendo vya rushwa katika taasisi za afya na jeshi la polisi, Jambo ambalo limekuwa limekuwa likizorotesha juhudui za serikali za kutoa huduma bora kwa wananchi.

Picha ya pamoja Viogozi wa dini wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kagaigai.

Pia viongozi hao wamemtaka Mkuu wa Mkoa huo, Stephen Kagaigai kuanza majukumu yake ya kwanza na suala la kudhibiti unywaji wa pombe za kienyeji aina ya gongo ambayo imekuwa ni changamoto kubwa katika baadhi za wilaya za mkoa wa huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wakati akitoa kero zao mbele ya mkuu huyo mpya wa mkoa,ambapo walisema kumekuwa na kero nyingi ambazo zimekuwa zikisababisha na watendaji wa zembe wasio jali wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya Askofu wa jimbo kuu katoliki la Moshi, Padre, Dk. Aidan Msafiri amesema vitendo vya rushswa Katika taasisi za umma vinapaswa kudhibitiwa kutokana na kwamba vimekuwa vikiathiri utendaji wa serikali Katika kuwa hudumia wananachi.

“Mkuu wa mkoa wakati umeingia hapa mkoani hapa tunaomba uanze na kushughulia masuala ya rushwa katika taasisi zetu za umma kwani baadhi ya watumishi wamekuwa wakisababisha serikali kusemwa vibaya na wakati tunajua juhudi za serikali katika utoaji wa huduma.

“Pamoja na tatizo hilo pia tatizo la unywaji wa pombe uliokithiri katika mkoa huo ni kubwa hali ambayo imekuwa ni changamoto kwa vijana kutojishughulisha na shughuli za maendeleo tunaomba utusaidie katika hili,”amesema.

Amesema suala la unywaji wa pombe za kienyeji aina ya gongo limekuwa ni changamoto kubwa hali ambayo imepelekea baadhi ya halmashauri za wilaya kupiga marufuku utengenezwaji wa aina hizo za pombe za kienyeji.

Askofu Mstaafu wa kanisa la Assemblies of God (TAG), Glorious Shoo, amesesema mbali na vitendo hivyo pia kumekuwa na vitendo vya unyanyasaji wa taasisi za elimu zinazomilikiwa na dini jambo ambalo limekuwa kikwazo kwa wananchi wengi katika shughuli za maendeleo.

Aidha alisema kumekuwa na suala la madada poa(wanawake wanaojiuza) ndani ya Manispaa ya Moshi imekuwa ni tatizo na kumuomba alishughulikie kwani imekuwa ni kero kwa jamii.

“Zipo changamoto nyingi kwenye taasisi za utoaji huduma kwa wananchi ikiwemo changamoto ya bima za afya ambapo wananchi wamekuwa hawapewi huduma na kutakiwa kulipa fedha na kutakiwa kutoa rushwa kupata huduma,”amesema Shoo

Hata hivyo Kagaigai aliwaahidi viongozi hao kuyafanyia kazi maombi hayo na kusema yale yote ambayo yako ndani ya uwezo wake atashughulika nayo ikiwemo suala la unywaji wa gongo huku akiwaomba viongozi hao wa dini kushirikiana naye katika kudhibiti hali hiyo.

“Hili niombe msaada kwa nyie viongozi wa dini najua mna nafasi kubwa sana ya kudhibiti hasa katika mahubiri wakati wa ibada ,sisi kama serikali tutapambana na changamoto hii lakini najua kabisa kupitia kwenu tunaweza kupunguza hili tatizo,”almesema Kagaigai.

Ameongeza kuwa viongozi hao wamemtaka kazinkubwa ya kufanya na kwamba ushauri wao imekuwa na manufaa makubwa kwa serikali Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zinazotahili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles