23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Selous Marathon kufanyika Agosti 21 Morogoro

Brighiter Masaki -Dar es Salaam

Shindano la riadha la Selous Marathon linalotarajia kufanyika Agosti 21, mwaka huu katika mkoa wa Morogoro, wameipa jina la Kijani Project.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi Imani Kajula, amesema kuwa mwaka huu itakuwa ya kitofauti kwa kuwa inafanyika mkoani Morogoro.

“Kwa mwaka huu mashindano haya tumeyapa nafasi ya kutangaza utalii wa nchi yetu kwa kuangalia vivutio mbalimbali”

“Kutakuwa na mazao mbalimbali pia kuna milima inayotililisha maji ambayo tunakunywa kutoka milima Uruguru.” amesema

Pia ameongeza kuwahakikishia ulinzi wa kutosha washiriki wote wa mbio hizo na pia tunawalipia bima ya maisha.

“Tunawalipia bima ya afya ya kuumia ambayo ni ya maisha itakayomuhudumia mshiriki kwa kipindi chote.”

Aidha ameongeza kuwa mbio za selous Marathon unapokimbia unapata medali ambapo kila mwaka unapata tofauti tofauti zinazokutambulisha mshiriki popote.

“Tunafanya mashindano haya kwanza ni mazoezi ilikusaidia afya zetu yanasaidia katika kuimarisha mwili na pia yanatangaza utalii wa ndani kwa kuwa wanashiriki na watu wa nchi zingine” amesema Kajula

Kwa upande wake Mgeni rasmi Jacob Nduye, amezindua wimbo wa Marathon ambao utatumika katika mbio hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles