24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MAJINA 11 YAMUUMIZA KICHWA TRUMP

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump tayari anayo orodha ya watu 11 anaowafikiria katika nafasi iliyoachwa wazi na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (FBI), James Comey, aliyemfukuza kazi.

Taarifa ya Ikulu ya nchi hiyo, White House, imesema hayo na tayari Idara ya Sheria imejiandaa kuanza usaili wa watu hao kuanzia jana.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Ikulu nchini humo, Sean Spicer, ametoa muhtasari kwamba Rais Trump atachagua mtu kujaza nafasi mara moja wakati atakapompata mtu anayekidhi vigezo muhimu vya kuiongoza FBI.

Hata hivyo, uteuzi huo utakuwa na uchunguzi wa kina kwa kuwa Comey alifukuzwa wakati akiongoza FBI kuchunguza iwapo kulikuwako na ushirikiano kati ya kampeni ya urais ya Trump na Russia mwaka 2016.

Wafuatao ni watu 11 ambao wanafikiriwa katika nafasi hiyo:

Ray Kelly

Awali alikuwa Kamishna wa Polisi wa Jiji la New York kwa muda mrefu kuliko mtu mwingine yeyote.

Mike Rogers

Ni mfanyakazi wa FBI ambaye ameshikilia pia nafasi ya Kiti cha Ubunge cha Michigan mpaka 2015 na pia amewahi kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Bunge.

Alice Fisher

Fisher alikuwa Naibu mwanasheria mkuu wa kitengo cha Jinai cha Idara ya Sheria, chini ya utawala wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, George W. Bush.

Trey Gowdy

Huyu ni mbunge kutoka Jimbo la South Carolina na pia aliwahi kuwa mwendesha mashtaka wa serikali kuu.

John Cornyn

Ni seneta wa chama cha Republican kutoka Jimbo la Texas na ni mwenye nafasi ya pili katika wadhifa wake kwenye Baraza la Seneti. Kabla ya hapo alikuwa mwanasheria mkuu wa Texas.

Paul Abbate

Amefanya kazi miaka mingi na FBI na hivi sasa anatumikia nafasi ya mkurugenzi mtendaji msaidizi wa Kitengo cha Jinai, Mitandao, Majibu na Huduma.

Michael Garcia

Alikuwa ni mwendesha mashtaka wa jiji la New York na hivi sasa anatumikia nafasi ya Jaji Msaidizi katika Mahakama ya Rufaa ya New York.

John Suthers

Suthers ni mwanasheria mkuu wa zamani wa Jimbo la Colorado na sasa ni meya wa mji wa Colorado Springs, katika jimbo hilo.

Michael Luttig

Luttig ni wakili wa zamani wa Idara ya Sheria na Jaji wa mahakama ya rufaa.

Larry Thompson

Thompson alikuwa naibu mwanasheria mkuu wa Marekani kati ya mwaka 2001 hadi 2003, wakati wa utawala wa Rais mstaafu George W. Bush.

Andrew McCabe

McCabe amekaimu ukurugenzi wa FBI katika kipindi cha wiki hii, baada ya Trump kumfukuza kazi Comey. Ni Naibu Mkurugenzi wa FBI.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles