28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

MAJIMAJI YAJAZWA NOTI ZA UDHAMINI VPL

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Sokabet imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini na klabu ya Majimaji kwaajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, wenye thamani ya Sh milioni 150.

Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo, Mwakilishi wa Kampuni ya Sokabet hapa nchini, Franco Ruhinda, alisema lengo la udhamini huo ni kurejesha kile wanachokipata kutoka wa jamii.

Ruhinda alisema udhamini wao kwa klabu hiyo ni mwanzo tu, kwani wamepanga mengi zaidi  ya hilo.

Alisema kampuni hiyo itakuwa inajihusisha na michezo ya kubashiri matokeo, lengo lake kubwa ni kuwawezesha Watanzania kupata fedha, kukuza michezo na kuchangia maendeleo ya kijamii.

“Kampuni hii ni ya Kitanzania yenye maskani yake jijini Dar es Salaam, itawawezesha washiriki kubashiri matokeo kupitia tovuti yake ya www.sokabet.co.tz, ambapo washiriki wanaweza kuvuna fedha nyingi hadi Sh milioni 100 kwa kubet kwa Sh 1,000 tu,” alisema Ruhinda.

“Licha ya Sokabet kuwawezesha washiriki wenye umri wa kuanzia miaka 18 kubet, pia inayo nafasi ya kukuza michezo kwa kuwekeza katika taasisi mbalimbali, mfano kwa kuanzia imeanza na klabu ya Majimaji ya Ruvuma.

“Ndani ya Sokabet kuna michezo mingi ya kubashiri, baadhi ni ‘American football, baseball, kikapu, kriketi, golf, mpira wa mikono, magongo ‘ice hockey’, mbio za magari, ragbi, tenisi, volleyball, ndondi na soka.”

Kwenye tovuti ya Sokabet, licha ya kushinda hadi Sh milioni 100 katika kipengele cha Sokabet Jackpot, pia washiriki wanaweza kubashiri matokeo kwa kuanzia Sh 200, ambacho ni kiwango cha chini kuliko makampuni mengine yote nchini.

Pia unaweza kuchagua lugha unayotaka kutumia kati ya Kiingereza au Kiswahili. Kuchagua lugha fungua tovuti kisha upande wa kulia juu bonyeza sehemu iliyoandikwa ‘Language’.

Mwenyekiti wa Majimaji, Steven Ngonyani, aliishukuru kampuni hiyo kwa udhamini huo, ambao alisema utaiwezesha timu yao kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles