29.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

KLOPP AMPANGA COUNTIHNO ULAYA

LONDON, England

KIUNGO wa Liverpool, Philippe Coutinho, jina lake limeorodheshwa katika orodha ya wachezaji wa timu hiyo watakaocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu mpya.

Kiungo huyo kwa sasa yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Brazil, iliyoko kwenye michezo ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia, inayotarajiwa kufanyika nchini Urusi mwakani.

Huenda uamuzi huo ukawa wa hatari kwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, kutokana na kiungo huyo kuomba kuondoka ili kujiunga na Barcelona.

Lakini Klopp amempanga kiungo huyo miongoni mwa wachezaji 25 watakaocheza Ligi ya Mabingwa msimu huu, ambao wataanza Septemba 13, Uwanja wa Anfield dhidi ya Sevilla.

Hatima ya kiungo huyo imeonekana kuwa gumzo ndani ya klabu hiyo katika wiki sita zilizopita.

Baada ya michezo ya kimataifa, timu za England, ikiwamo Liverpool, Manchester City na Chelsea kwa pamoja zinatarajia kutuma ndege kuwachukua wachezaji wao ili kuiwahi michezo ijayo ya Ligi Kuu.

Hata hivyo, si mara ya kwanza kwa Liverpool kutuma ndege binafsi kumchukua Coutinho, kwani walifanya hivyo msimu uliopita ili kuepuka usumbufu kwa mchezaji wao.

Lakini Klopp anatakiwa kufanya uamuzi mzito katika kupanga kikosi chake kuelekea mchezo wake wa ugenini wa  Ligi Kuu dhidi ya Manchester City wiki hii.

Coutinho hakupangwa katika kikosi cha Liverpool tangu msimu uanze na tayari ameeleza lengo lake la kutaka kuhama Liverpool na kujiunga Barcelona.

Lakini inaonekana kuwapo nafasi finyu  kwa Klopp kumpanga Coutinho katika kikosi chake, kitakachosafiri hadi Uwanja wa  Etihad, kucheza dhidi ya Manchester City.

Coutinho hakuwapo kwenye kikosi kilichoifunga Arsenal mabao 4-0 katika mchezo wao wa mwisho, lakini Klopp atalazimika kumfanyia majaribio wakati atakaporejea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,692FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles