25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

MAJANGILI TISA JELA MIAKA 25

jail

Na MALIMA LUBASHA -SERENGETI

MAHAKAMA ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, imewahukumu watu tisa kifungo cha miaka kati ya 20 na 25 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya ujangili na kupatikana na silaha kinyume cha Sheria.

Akitoa hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile, aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Juma Mahende, Yohana Range, Meshack Philemon, Michael Bukuru na Amos Alexander ambao kwa pamoja wamehukumiwa kifungo cha  miaka 25 jela kila mmoja kwa kupatikana na nyara za Serikali zenye thamani ya Sh milioni 29.6.

Hakimu Ngaile alifafanua kuwa baadhi ya washtakiwa hao walitiwa hatiani kwa makosa ya kupatikana na meno ya tembo, ngozi ya pundamilia, swala na nyumbu kinyume cha sheria.

Alisema washtakiwa Sudi James na Nyaburu Wambura, wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa kukutwa wakiwa na bunduki na risasi kinyume cha sheria za nchi.

Aidha mshtakiwa Jackson Nyamirobe, alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela  kwa kosa la kupatikana na ngozi za pundamilia, swala na nyumbu ikiwa na kuingia ndani ya eneo la hifadhi, huku Boke Mwita alihukumiwa  kifungo cha miaka mitano jela kwa kukutwa akiwa na mifupa ya tembo.

Hakimu Ngaile, alisema adhabu hiyo imetolewa baada ya kuridhika na ushahidi pamoja na vielelezo vilivyotolewa mahakamani.

Awali, mwendesha Mashtaka wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Emmanuel Zumba, alisema washtakiwa walikuwa  wanakabiliwa na kesi nne tofauti. Kwamba walifanya makosa hayo kati ya Novemba 2, 2014 na Mei 2, mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles