22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AZUIA USHURU KABLA YA KUNUNUA MAZAO

Na CLARA MATIMO


 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amepiga marufuku halmashauri zote nchini kuwatoza wanunuzi wa mazao ushuru wa huduma kabla ya kununu mazao hayo.

Agizo hilo alilitoa juzi alipozungumza na wadau wa zao la pamba wakiwamo wakulima, wataalamu wa kilimo, wanunuzi na wamiliki wa vinu vya kuchambua  pamba.

Wengine ni watendaji kutoka Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Waziri wa Fedha, taasisi za fedha na viongozi mbalimbali wakiwamo na wakuu wa mikoa ya Mwanza, Geita Tabora, Simiyu na Mara.

Alisema kuanzia msimu huu   wa kilimo cha pamba, kila mfanyabiashara anayenunua zao hilo hapaswi kulipa fedha taslimu kama ilivyokuwa zamani ambako wanunuzi walikuwa wakilipa fedha taslimu hivyo kuleta mgogoro baina ya wafanyabiashara na halmashauri hizo.

Majaliwa alisema katika utaratibu wa zamani wafanyabiashara walikuwa wakilipia fedha lakini wakati mwingine walikuwa wanaweza kukwama kununua pamba.

Alisema wafanyabiashara  wamekuwa wakikwama kurejeshewa fedha zao hivyo ameamua kufuta utaratibu huo na badala yake watalipa wanaponunua kulingana na kiasi walichonunua.

“Mfanyabiashra anaweza kulipa kiasi fulani cha fedha, lakini akienda kununua anakosa kufikia kiwango alichokuwa anakitaka na fedha zote za serikali huwa zina matumizi, zikiingia wakurugenzi huzipangia matumizi tayari,” alisema.

Waziri Mkuu alisema  ushuru  wa mazao   anaopaswa kulipa mfanyabiashara ni asilimia tatu ya kile alichonunua.

Kwa sababu hiyo  aliwaonya wakurugenzi kutoendelea na utaratibu wa zamani akisema  serikali italisimamia hilo kwa lengo la kulinda mitaji  wa wafanyabiashara.

Hata hivyo aliwataka wakurugenzi wote ambao wanadaiwa ushuru huo na wanunuzi wa zao hilo katika msimu uliopita, wafanye utaratibu wa kuwalipa fedha zao  kuondoa migogoro.

Waziri Majaliwa alisema atakutana tena na wanunuzi   na wadau wa zao hilo kabla ya msimu kuanza Mei Mosi mwaka huu ili wapange bei.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,169FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles