22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

PROF. MUHONGO AGAWA MBEGU ZA ALIZETI

Na SHOMARI BINDA


MBUNGE wa   Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, amegawa bure kilo 6,318 za mbegu za alizeti na ufuta   zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 24 kwa wakulima 4000 wa jimbo lake kama mazao ya  iashara   waweze kuondokana na umasikini.

Mbegu hizo alizigawa kwenye vituo vitano  vya kata za Bulinga, Suguti, Bugwema, Tegeruka na Nyegina.

Alisema huo ni msimu wa tatu wa kugawa mbegu bure kwa wakulima kwenye jimbo lake ikiwa ni jitihada za kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Alisema msimu huu utakuwa na tofauti ambako hatua hiyo  itasimamiwa na mkuu wa wilaya ya Musoma kuhakikisha wakulima wanaopata mbegu hizo wanapanda na kufuatiliwa mashamba yao kuona mafanikio yanapatikana.

Muhongo alisema lengo ni jema la kugawa mbegu kwa wananchi vijijini.

Hata hivyo alisema  wapo wanaopokea mbegu hizo lakini wanashindwa kuzipanda hivyo msimu huu kutakuwa na usimamizi mzuri na ufuatiliaji kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya na maofisa kilimo wa halmashauri ya Musoma.

“Nimekuwa nigawa mbegu hizi hususani za alizeti kwa misimu miwili bure kwa wananchi lakini nashukuru kipindi hiki halmashauri ya Musoma nayo imechangia kwa kuleta mbegu za ufuta na hii yote ni kuwajali nyie wananchi muweze kuondokana na umasikini.

“Kipindi cha nyuma mlikuwa mkijisimamia wenyewe lakini kipindi hiki hatua nzima ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji utafanywa na mkuu wa wilaya ambaye nimeafuatana  naye   kuhakikisha mbegu zinazogawiwa zinapandwa na kuleta tija kwa wananchi,”alisema Muhongo.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano, alisema katika kuhakikisha ufuatiliaji wa karibu unafanikiwa kila mkulima atakayepata mbegu hizo ataandikwa jina na kutoa mawasiliano yake ikiwemo eneo la shamba lake lilipo waweze kufuatiliwa na kukagua mashamba yao.

Alisema   Profesa  Muhongo, amekuwa akifanya jitihada kubwa katika kuwainua wakulima na kuona wanapata mafanikio hivyo serikali itafuatilia na kuunga mkono juhudi hizo ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri na elimu kwa wakulima.

Naano alisema ni gharama kubwa ambazo zimetumika kununua mbegu hizo na kugawiwa wakulima.

Aliwaonya wakulima ambao  hawataweza kupanda mbegu hizo kuacha kuzichukua na kuwaachia wenye mahitaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,167FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles