22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AONYA MIGOGORO YA WAKURUGENZI, MAMEYA

Na CLARA MATIMO-MWANZA


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amezionya halmashauri za jiji, wilaya na miji zenye migogoro, kuanza kuitatua haraka kabla hajafika ili zibaki na jukumu la kuwatumikia wananchi.

Pia, Waziri Mkuu Majaliwa amepiga marufuku watumishi wa Serikali wenye kampuni binafsi kuchukua zabuni serikalini.

Akizungumza na watumishi, watendaji, madiwani na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya za Ilemela na Nyamagana, mkoani Mwanza jana, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuna taarifa za kuwapo kwa migogoro katika halmashauri nyingi nchini kati ya mameya na wenyeviti pamoja na wakurugenzi watendaji.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, sehemu kubwa ya migogoro hiyo, inasabababishwa na maslahi binafsi.

“Katika halmashauri nyingi nilizotembelea, nimekutana na migogoro inayosababisha watumishi na watendaji kuwa katika makundi, hivyo kushusha kiwango cha uwajibikaji na kuwakosesha maendeleo wananchi.

“Sasa, nikiwa kama mtendaji mkuu wa Serikali, nawaeleza wale wenye migogoro, kaeni mtafute namna ya kupata ufumbuzi wa migogoro yenu maana sasa sitowavumilia.

“Sitaki kusikia ikiendelea tena kwa sababu mnakuwa na migogoro mnashindwa kuzingatia itifaki zilizopo za maadili ya uongozi na watumishi wa umma.

“Mnakuwa na migogoro kwa sababu wakati mwingine mnachukua zabuni za halmashauri mnazozifanyia kazi wakati mkijua hairuhusiwi.

“Kutokana na uwepo wa migogoro mingi na inayojikita kwenye maslahi binafsi, nimeamua kupiga marufuku watumishi wa Serikali wenye makampuni yao binafsi, kuchukua zabuni mbalimbali katika halmashauri yoyote hata kama siyo anayoifanyia kazi kwa kuwa wamekuwa wakipewa upendeleo usiofaa.

“Hapa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, mlikuwa na mgogoro uliotokana na maslahi binafsi, nashukuru mmeumaliza baada ya Mheshimiwa Rais John Magufuli kuagiza muutatue.

“Lakini, kama bado kuna chembechembe zimebakia, naomba zimalizeni mapema ili mbaki kuhudumia wananchi,” alisisitiza.

Hata hivyo Majaliwa aliwataka wakuu wa idara kuacha tabia ya kuwadharau madiwani na kwa kuwa wawakilishi hao wa wananchi wapo kwenye halmashauri zao kama watumishi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles