26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

WANASAYANSI: TRUMP RAIS MBAYA ZAIDI KATIKA HISTORIA YA MAREKANI

WASHINGTON, MAREKANI


WANASAYANSI waandamizi karibu 200 wa Marekani wamepiga kura ya kumwonyesha Rais Donald Trump kuwa Rais mbaya zaidi katika historia ya Marekani.

Kwa mujibu wa Utafiti wa Ukuu wa Marais na Watendaji wa kisiasa wa 2018, Trump alitupwa hata na Rais aliyetia aibu kwa kashfa, Richard Nixon ambaye pia alipingwa na wahafidhina huku Abraham Lincoln akiongoza. Nixon alishika nafasi ya 33.

Utafiti unaofanyika kila baada ya miaka minne huwahoji wanasayansi wa kijamii wa Chama cha Sayansi ya Siasa Marekani kupitia kitengo chake cha marais na watendaji wa kisiasa.

Huwauliza wataalamu hao kuorodhesha ukuu wa kila rais katika alama kuanzia sifuri hadi 100, huku 100 ikiwa ukuu, 50 wastani na 0 kushindwa kabisa.

Wastani wa alama aziyopata Trump ni 12.34 hivyo kumtoa mkiani James Buchanan – aliyedumu kwa miaka mingi kama rais mbaya kabisa katika historia ya taifa hilo baada ya kuiingiza Marekani katika vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Matokeo hayo yanakuja miezi michache tu baada ya Trump kumaliza mwaka wake wa kwanza madarakani kama rais asiyependwa zaidi katika historia ya kisasa.

Mtangulizi wa Trump, Barack Obama aliruka nafasi 10 tangu utafiti wa mwisho ufanyike mara ya mwisho mwaka 2014 na kushika nafasi ya nane huku aliyemtangulia George W Bush pia akipanda katika orodha hiyo kwa nafasi tano kufikia alama 30.

Bill Clinton alishuka kwa nafasi tano na kuwa wa 14 huku Andrew Jackson akishuka zaidi kwa nafasi sita, pengine kutokana na ongezeko la mtazamo hasi wa namna alivyowatendea Wamarekani asilia.

Marais saba walioshika nafasi za juu wamebakia katika nafasi zao ni Abraham Lincoln akifuatiwa na George Washington, Franklin Delano Roosevelt, Theodore Roosevelt, Thomas Jefferson, Harry Truman na Dwight Eisenhower.

Trump alisindikizwa na walioshika nafasi tano za mkiani ambao ni Andrew Johnson, Franklin Pierce, William Harrison na Buchanan.

Wakati watafiti hao ambao wanajumuisha wenye mrengo wa Democratic na Republican au huru wakitofautiana namna wanavyowatazama viongozi kama Obama na Bush, walikubaliana kwa kiwango kinachokaribiana sana kuhusu Trump.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles