22.4 C
Dar es Salaam
Sunday, May 12, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa aiagiza TCAA kuzuia matumizi mabaya viwanjani

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), kuimarisha mifumo ya udhibiti wa matumizi mabaya ya viwanja vya ndege nchini ili visiwe vichochoro vya kusafirishia bidhaa haramu.

Pia ameitaka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESBL) kufanya marejeo ya viwango vya mikopo vinavyotolewa kwa wanafunzi wa urubani na kutoa kipaumbele kwa wahitaji wa fani za masuala ya usafiri wa anga.

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Oktoba 30,2023, jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA yaliyowakutanisha wadau mbalimbali.

Amesema tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003 malengo yalikuwa ni kuthibiti na kusimamia huduma za usafiri wa anga nchini.

“TCAA imarisheni mifumo ya udhibiti wa matumizi mabaya ya viwanja vya ndege kuhakikisha havigeuki kuwa vichochoro vya kusafirishia bidhaa haramu ili nchi iendelee kuwa na sifa ya kuwa kati ya nchi zenye udhibiti mzuri wa anga ,” amesema Majaliwa.

Ameitaka mamlaka hiyo kujifunza kutoka mataifa yaliyofanikiwa kwa kuiongeza viwango vya utoaji wa huduma, ubunifu na kuweka mikakati ya kuimarisha soko.

Amesema wadau wa usafiri wa anga wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo inayosimamia sekta hiyo.

Ameongeza kuwa TCAA kuendelea kubuni na kuongeza vyanzo vipya vya mapato ya ‘Aviation Training Fund ‘ ili kuongeza idadi ya marubani wanaopata ufadhili wa masomo.

“Watanzania endeleeni kuviamini na kutumia vyuo vilivyopo nchini kwani vinatoa mafunzo ya utalaamu wa anga wa uhakika,”amesema.

Amesema serikali imepanga kuimarisha sekta ya anga kwa kuwezesha ununuzi wa rada za kisasa nne za kuongoza ndege za kiraia ambazo zimefungwa katika viwanja vya ndege vya mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro na Songwe.

Naye Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameipongeza TCAA kwa kusimamia ukaguzi na kuiweza nchi kupata alama 86.7 katika viwanja vya Dar es Salaam na Zanzibar.

Amesema serikali imeboresha miundombinu mbalimbali ya viwanja vya ndege hivyo kutokana na maboresho hayo anaamini ukaguzi ujao nchi itafikia asilimia 90.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TCAA, Hamza Johari, amesema kuwa mamlaka hiyo inaendeshwa kwa kutumia mapato ya ndani haitegemei ruzuku serikalini.

“Kwa miaka mitano tumekusanya bilioni 319.9 ambapo bilioni 24.5 tumechangia katika mambo mbalimbali ya kijamii,”amesema Johari

Amesema TCAA imefungua mikataba mbalimbali ya usafiri kwa nchi 80 hivi karibuni wameingia mkataba na nchi ya Marekani hivyo kuziwezesha ndege ya Air Tanzania kwenda kwenye nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles