28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Haloteli yazindua huduma mpya

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya mawasiliano ya haloteli, imezindua huduma mpya inayoitwa ‘Kivumbi na Haloteli’ ambapo wateja wake watajishindia zawadi mbalimbali ikiwa ni katika kusherehekea miaka nane tangu kuanzishwa kwake hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Oktoba 30,2023, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja, Patrick Rwegashora, amesema katika sherehe hiyo ya miaka nane wanatambua mafanikio yao yametokana na imani, uamimifu wa wateja kwa kutumia mtandao huo.

Amezitaja zawadi zitakazotolewa kuwa ni kupitia kampeni hiyo ni gari aina ya Mazda 5CX simu janja aina ya samsung galaxy A 345G na M14 na router zote zikiwa na laini za haloteli zenye bando la GB 5-10.

“Kushiriki katika promosheni hii inayolenga wateja wetu wa halotel unatakiwa kununua vocha ya kukwangua yenye thamani ya kuanzia 2000 au zaidi kwa kujiunga na kifurushi pia kupitia huduma ya halopesa,” amesema Rwegashora.

Ameongeza kuwa promosheni hiyo inalenga wateja wote walioko nchi nzima lengo kuu ni kutoa shukrani kwa watanzania kwa kuendelea kuunga mkono na kutumia mtandao huo katika miaka nane.

Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Masoko Halopesa, Roxana Kadio, amesema kuwa wateja wanahimizwa kushiriki kikamilifu na kutumia fursa hiyo ili kuweza kujishindia zawadi hizo ambapo kampeni hiyo itadumu kwa miezi mitatu kuanzia Oktoba 2023.

“Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel ikiwa kama sehemu ya huduma kwa wateja ni wajibu wetu kuja na shukrani kwa wateja wetu ili kuendeleza mahusiano kwa watanzania wote nchi nzima” amesema Roxana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles