24.8 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

IWPG yataka kusitishwa kwa vita Israel na Hamas

Na Mwandishi Wetu

KUNDI la Kimataifa la Amani la Wanawake (IWPG),limetaka kusitishwa mara moja kwa mapigano yanayoendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 26,2023 na kundi hilo kuhusu vita ya Israel na Hamas, limehimiza kusitishwa kwa mzozo huo wa kijeshi na kufanyika kwa makubalino ya amani.

“Hakuna sababu ya kimaadili inayoweza kuhalalisha kitendo cha kuwashikilia raia wasio na hatia kama mateka. Wanawake, vijana na watoto wanaathiriwa na uharibifu wa vita.

Imesema kuwa kwa kutambua madhara ya kulipiza kisasi, inazitaka pande zote mbili kusitisha uhasama huo haraka na kushiriki katika mazungumzo yenye kujenga kwa ajili ya amani.

” Iwapo mzozo huu utaendelea, idadi ya waliopoteza maisha inakadiriwa kufikia mamilioni. Madhara ya ukatili na uharibifu huo hayawezi kupimika, na hakuna fidia inayoweza kufidia ipasavyo gharama ya mwanadamu,” imesema taarifa hiyo.

Shirika hilo lisilo la kiserikali lililo katika mashauriano na Baraza la Umoja wa Mataifa la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) na lililosajiliwa chini ya Idara ya Mawasiliano ya Kimataifa (DGC) linatoa wito kwa Jumuiya za Kimataifa, ikiwa ni pamoja na UN, kuchukua hatua za haraka na zinazofaa ikiwamo utoaji wa misaada ya kibinadamu .

Vita vya Israel na Hamas vilianza kwa Hamas kuanzisha mashambulizi dhidi ya Israel Oktoba 7,2023, ilikuwa ni vita vya kwanza kwa pande mbili katika kipindi cha miaka tisa tangu mzozo wa Gaza wa mwaka 2014.

“IWPG inashutumu kila aina ya uhalifu wa kivita na vitendo vya unyanyasaji vinavyovuruga amani ya dunia na imejitolea sana kufikia amani ya dunia na wanawake duniani kote,”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles