22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Mahusiano yako yanapaswa yawe namna hii

NDANI ya ulimwengu wa mapenzi kuna kitu ambacho ni vyema kila mtu akakijua. Kila mmoja katika mapenzi  anapaswa kuwa na njaa na mwenzake. Yaani ampende, amjali na awe na hofu kumpoteza.

  Ikiwa mmoja anaonekana ana hofu zaidi ya kumpoteza mwenzake, huku mwingine akiona hilo si jambo baya, ni vyema ukajiuliza. Kwanini hali iko hivyo? Mapenzi ni suala linalotakiwa kuhusisha pande zote mbili. Baina ya mwanamke na mwanaume.

 Kama mwanaume ndiye anaonekana anashida sana na mwanamke, hapo kuna walakini. Na hata mwanamke anapoonekana kuwa ni yeye mwenye shida sana na mwenzake, hapo pia kuna walakini.

 Japo kitaalamu hapo kunaweza kuwa na sababu nyingi, ila hapa tuone thamani na maana ya kila mmoja kuwa na uhitaji na mwenzake. Uhitaji huu hasa huwa katika maana ya mapenzi, japo pia wengine wanaweza kuwa na uhitaji kwa fulani kwa sababu tofauti ikiwemo suala la kipato. Tuangalie thamani ya kuihitaji katika namna ya kimapenzi. Kama mtu hakupendi hawezi kuwa na uhitaji na wewe.

 Kama mbali na kila matendo mazuri unayomfanyia haoni hatari kuwa na mbali na wewe, kuna jambo. Mapenzi ni suala linalohitaji uwepo wa unayempenda. Bila kujali gharama au umbali kila mmoja uhitaji kuwa karibu na mtu ampendaye. Ni vipi fulani aseme anakupenda ikiwa haathiriki na kuachana kwenu?

Si vyema kujidanganya, ukweli ni kwamba hakuna anayetaka kuwa mbali na mtu anayempenda kwa dhati. Kama kila unalotakiwa kumfanyia, unamtendea. Kama kauli zako kwake ziko vizuri. Ikiwa tabia yako haina mashaka na unamfanya kuwa bora na wa kipekee katika maisha yako. Ni kwa namna gani kama anakupenda apende uachane nawe?

 Najua kuna watu wako radhi kuachana na watu wanaowapenda kutokana na tabia fulani za wahusika. Ila hii hutokea kama anayependwa haonekani kujali wala kuthamini upendo wa mwenzake. Hata siku moja anayekupenda hawezi kutamani kuachana na wewe ikiwa uko katika tabia njema na za kupendeza.

Huyo anayetaka muachanye naye, mtazame vizuri. Kweli anakupenda? Na kama kweli anakupenda ni furaha ipi ataipata kama akiachana na yule ampendaye? Anayekupenda hata siku moja hawezi kutaka kuachana na wewe.

 Atahitaji uwe karibu yake, apate pendo lako na furaha ya maneno yako. Bila kuwaza sana ila huyo anayependa muachane jua kuna suala na uhaba wa mapenzi katika nafsi yake juu yako. Ni nani hapendi furaha? Na iko wapi furaha katika mapenzi kama furaha ya kuwa na mtu unayempenda?

    Kwa ajili ya mapenzi yao kwa akina fulani baadhi wako radhi kufanya kila kitu na kwenda kila mahali kwa ajili ya kunusuru penzi lao. Vipi fulani awe anakupenda na bado apende kuwa mbali na wewe?

 Ni uongo na wala haiwezi kuwa kweli. Daima anayekupenda atahitaji kuwa karibu na wewe. Akujali. Akuthamini na aone thamani ya maisha yako kama anavyoiona fahari ya maisha yake. Mapenzi si suala haba. Ni suala maalum na linalogusa mahala maalum.

 Hakuna anayetaka kuwa mbali na suala hili, hasa baada ya kuwa na mtu anayempenda. Ukiona mbali na mazuri yako anahitaji kuchana na wewe, ujue hujamgusa mahala, mahala maalum katika nafsi yake na katika maisha yake na ndiyo maana anahitaji kuachana na wewe.

  Acha kutumia nguvu nyingi kumvuta. Mapenzi yana nguvu ikiwa utakuwa mwema sana kwake. Kama baada ya kila kitu kizuri hakuhitaji, jua mti uliotua siyo mufaka kwa ndege wa aina yako. Anza safari!

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles