23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 10, 2022

Mkosi wa Drake balaa, cheki alichowafanya wachezaji hawa

CHRISTOPHER MSEKENA

UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya  Aubrey Graham maarufu kama Drake, rapa na mwimbaji bora zaidi duniani kwa sasa ambaye wiki hii, amekuwa gumzo katika ulimwengu wa soka na burudani.

Drake, raia wa Canada hivi sasa yupo Ulaya akiendelea na ziara yake Assassination Vacation ambayo imekuwa na mafanikio makubwa kwa kujaza mashabiki katika viwanja mbalimbali barani humo ukiwamo ule wa The O2 Arena uliopo jijini London.

AS ROMA WAMLIPUA DRAKE

Jumatatu wiki, klabu ya AS Roma ya Italia iliwapiga marufuku wachezaji wake kupiga picha na Drake mpaka msimu huu uishe ili kukwepa kile ambacho mashabiki  wa muziki na soka wamekiita mkosi.

Katazo hilo lililotolewa katika ukurasa wao wa Twitter, lilikuja mara baada ya kuwapo kwa mfululizo wa wachezaji wa vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi za Uingereza kushindwa kufanya vizuri na timu zao kufungwa mara baada ya kupiga picha na rapa huyo.

JADON SANCHO

Machi 11, mwaka huu mchezaji kinda wa Uingereza katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, aliweka picha aliyopiga na Drake wakifurahi pamoja. Baada ya mchezo huo timu yake ikafungwa mabao 5-0 na Bayern Munich.


JADON SANCHO NA DRAKE

AUBAMEYANG, MESUT OZIL

Aprili 2 mwaka huu katika uwanja wa burudani wa The O2, Drake alikuwa na onyesho lake lililohudhuriwa na mastaa mbalimbali wa soka. Miongoni mwa wachezaji waliopiga picha na Drake ni Pierre Aubameyang mshambuliaji wa Arsenal na nahodha wa timu hiyo Mesut Ozil kisha timu yao ikafungwa bao 1-0 na Evarton.

SERGIO AGÜERO

Mshambuliaji huyu wa Manchester City naye ameingia kwenye orodha hii ya mkosi wa Drake mara baada ya Machi 11 kupiga picha na rapa huyo, kisha akakosa penati na timu yake ikafungwa bao 1-0 na Tottenham.

Hali kadharika katika mchezo wake uliofuata ikafugwa mabao 4-3 na Tottenham hivyo ikatolewa kabisa katika ligi ya mabingwa Ulaya.

PAUL POGBA

Katika uwanja wa Manchester Arena, Drake alikuwa na onyesho lake, Machi 11 na mastaa mbalimbali walikuwamo kushuhudia burudani, ndipo mchezaji wa Manchester United, Paul Pogba alimfuata Drake nyuma ya jukwaa na kupiga naye picha akimkabidhi jezi.

Pogba na Drake

Kilichofuata hapo ni timu yake kupoteza mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa kwa kuchapwa bao 1-0 na Barcelona jambo ambalo mashabiki wengi waliona wametiwa mkosi na Drake baada ya mchezaji wao kupiga naye picha.

LAYVIN KURZAWA

Mchezaji huyu wa Kifaransa anayekipiga katika klabu ya PSG, naye alisombwa na mkosi wa Drake mara baada ya kuhudhulia onyesho lake lililofanyika uwanja wa The 02 na kupiga naye picha kisha timu yake ikachapwa mabao 3-2 na Fc Nantes.

MASHABIKI WAFUKUA MAKABURI

Kuna binadamu katika mitandao ya kijamii hawapendi utani kabisa. Katika ishu hii ya Drake wamerudi nyuma mpaka mwaka 2015 ambapo mchezaji wa tenisi, Serena Williams alipoteza mchezo wake muhimu dhidi ya Roberta Vinci.

Kushindwa kwa mchezo huo kulifanya Serena, akose ushindi ambao ungemuweka kwenye rekodi kubwa zaidi katika tenisi sawa na ile iliyowahi kuwekwa  mwaka 1988 na Steffi Graf.

Hiyo yote ilitokana na Drake kuwapo katika viwanja vya Grand Slams kushuhudia mchezo huo kwani kipindi hicho Serena na rapa huyo walikuwa wapenzi.

CONOR MCGREGOR
Mwaka 2018, mwana masumbwi maarufu duniani kutoka Ireland, Conor McGreror alichapwa ngumi na kupoteza pambano katika mzunguko wanne na bondia wa Kirusi, Khabib Nurmagomedov ikiwa ni muda mfupi toka aweke picha kwenye mtandao wa Instagram akiwa amepiga na Drake.


Conor McGreror na Drake

NI MKOSI AU UTANI?
Ishu hii inatumiwa zaidi na mashabiki kama utani wa kuunganisha matukio ya wanamichezo hawa waliopiga picha na Drake kisha wakapoteza michezo yao kwani haina ushahidi wa kitaalamu kama kuna uhusiano wowote wa picha za Drake na kushindwa kwao.
Ndiyo maana katika mitandao ya mastaa hao, mashabiki wameanzisha kampeni ya utani ya kufuta picha zote ambazo walipiga na rapa huyo anayefanya vyema sokoni na albamu yake, Scorpion.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles