25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA YAZUIA AGIZO LA TRUMP DHIDI YA WAHAMIAJI

WASHINGTON, MAREKANI


JAJI wa Mahakama Kuu nchini Marekani, Ann Donnelly ametoa uamuzi kupinga agizo la Rais Donald Trump la kuwazuia wasafiri kutoka nchi sita; Syria, Somalia, Sudan, Libya, Yemen, Iran na Irak kuingia Marekani.

Akitoa uamuzi huo jana, Jaji huyo aliamuru wale walio na hati halali za kuingia hapa waruhusiwe kuingia au kuendelea na safari zao.

Jaji Donnelly ameagiza serikali itoe orodha ya wote wanaozuiwa viwanja vya ndege  na kwamba kitendo hicho kinachotokana na agizo la Rais, kunawaathiri vibaya.

Maafisa wa usalama wa ndani na uhamiaji wamesema bado hawajaona agizo hilo la mahakama lakini wameahidi kuliheshimu.

Zaidi ya wasafiri 100 wamekwama katika viwanja kadhaa vya ndege nchini Marekani kutokana na agizo hilo la Trump.

Hali hiyo iliyalazimu makundi ya kutetea haki za binadamu na asasi za kiraia za hapa kuandaa maandamano katika viwanja vya ndege kupinga agizo hilo na kufungua kesi mahakamani.

Agizo hilo la Trump lililotiwa saini siku ya Ijumaa linasitisha mpango wa wakimbizi kwa siku 120 zijazo, kusitisha utoaji wa visa na kuzuiwa kwa wasafiri kutoka nchi kadhaa za Kiislamu kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Wakati wa kampeini, Trump aliahidi kuchukua hatua za kukabiliana na ongezeko itikadi kali na kitisho cha ugaidi ili kuwalinda Wamarekani dhidi ya mashambulizi hayo.

Lakini juzi, kiongozi huyo alikanusha kuwa agizo hilo ni marufuku kwa Waislamu kuingia Marekani, akisema ni hatua ambazo muda wake umewadia na kuwa limeanza kutekelezwa vizuri kama inavyoshuhudiwa katika viwanja vya ndege.

Trump pia ameliagiza Jeshi la Marekani kuwasilisha mkakati mpya wa kupambana na kundi lijiitalo Dola la Kiislamu (IS) katika kipindi cha siku 30 zijazo.

Wiki moja tangu kuingia madarakani, kiongozi huyo mpya wa Marekani ametia saini maagizo 18, mengi yao yakiutikisa ulimwengu na kuwaathiri mamilioni ya watu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles