26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

WAFUASI 200 CHADEMA WATUA CCM

Na Mwandishi Wetu-Lushoto


CHAMA  cha  Demokrasia  na Maendeleo (Chadema), kimeendelea  kupata  pigo  baada  ya  wanachama  200, wakiwamo  viongozi  wa Kitongoji  cha Kwemghogho Mahezangulu kujitoa  na  kujiunga  na  Chama Cha Mapinduzi (CCM) .

Akizungumza  baaada ya  kupokea  wanachama  hao, Mbunge wa  Bumbuli, January Makamba (CCM),  alisema  wananchama  hao  wameamua  kurudi  wenyewe nyumbani   kutokana  na   kuona  ahadi  nyingi  za maendeleo zimetekelezwa  kwa  kiasi kikubwa.

Alisema  chama  chake kimefanya mambo mengi  hivyo  haoni  ajabu  ya  kupokea  wanachama kutoka  vyama  vingine  vya  upinzani.

January, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, alisema  hivi sasa kuna kazi kubwa ya kuendelea kuleta maendeleo ambayo yanahitaji umoja  na mshikamano.

Alisema migogoro, majungu na fitina inatokana na kambi  zilizokuwapo huku akiwasisitiza wana CCM watambue ni hema kubwa na linavumilia tofauti za watu.

Aliyekuwa  Mwenyekiti wa  Chadema  Kitongoji cha Kwemghogho, Shabani Kahema,  aliwataka   vijana  na  wanachama  wengine  kubadilika kwa kuwa CCM ndiyo chama chenye ilani inayotekelezeka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles