22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yatishia kufuta kesi ya Lema

lemaaNa  JANETH MUSHI, ARUSHA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, imetishia kuzifuta kesi mbili zinazomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), ikiwemo kesi ya kusambaza ujumbe unaomkashifu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Augustine  Rwezile, baada ya upande wa mashtaka kuomba uongezwe muda wa siku 60 kwa ajili ya kukamilisha upelelezi wa kesi hizo.

Akizungumza baada ya upande wa mashtaka kuomba siku hizo, Hakimu Rwezile alisema kama upande wa mashtaka utashindwa kukamilisha upelelezi baada ya siku hiyo, mahakama hiyo itachukua uamuzi wowote ikiwa ni pamoja na kuifuta kesi.

“Naahirisha kesi hii hadi Novemba 15 mwaka huu, kwa ajili ya kuja kusoma maelezo ya awali ya mtuhumiwa, lakini siku hiyo mkisema upelelezi haujakamilika, mahakama itafanya uamuzi wowote ikiwamo kuifuta kesi
hii,” alisema Hakimu Rwezile.

Awali, Wakili wa Serikali, Blandina Msawa, alidai mahakamani hapo kuwa bado hawajakamilisha upelelezi, hivyo hawataweza kumsomea Lema maelezo ya awali na mahakama hiyo iwape muda wa siku 60 kwa ajili ya kukamilisha upelelezi huo.

Kwa upande wake, Wakili wa Utetezi, John Mallya, alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo ni rahisi kwani tangu Lema akamatwe na polisi na kufikishwa mahakamani, simu yake ya mkononi inashikiliwa hadi sasa.

“Upelelezi wa kesi hii uko ‘very simple’, kwani simu ya Lema mpaka sasa mko nayo mnaichunguza. Kwa hiyo, nashangaa kwanini upelelezi haukamiliki kwa wakati ili mteja wangu asomewe maelezo ya awali,” alihoji Wakili Mallya.

Katika kesi ya kwanza, Lema anadaiwa kusambaza ujumbe unaomkashifu Gambo kati ya Agosti 20 mwaka huu, mkoani Arusha, huku akijua ni kosa kisheria.

Katika kesi ya pili, Agosti mosi hadi Agosti 26 mwaka huu, Lema anadaiwa kurusha maneno ya sauti kwa njia ya mtandao wa WhatsApp yanayodaiwa kukusudia kuishawishi jamii iandamane Septemba mosi mwaka huu, huku akijua ni kosa kisheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles