25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yampa Musiba siku saba kesi dhidi ya Membe

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,  imempa siku saba mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba na wachapishaji wa gazeti hilo wawe wamewasilisha majibu dhidi ya madai ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe anayetaka kulipwa Sh bilioni 10 kwa kuchafuliwa.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa leo Jumanne Julai 2, mbele ya Jaji Joaquine Demelo baada kupitia maombi ya wajibu maombi ya kutaka waongezewe muda wa kuwasilisha utetezi na majibu kinzani.

Jaji Demelo amesema wajibu maombi walitakiwa kuwasilisha utetezi na majibu kinzani ndani ya siku 21 baada ya shauri kufunguliwa Desemba mwaka jana lakini hawakufanya hivyo ambapo Musiba kupitia Wakili wake Majura Magafu waliomba kuongezewa muda japo wadai walipinga maombi hayo wakitaka yasikubaliwe.

“Mahakama imesikiliza hoja za pande zote mbili imeona kesi ina maslahi kwa umma hivyo ni bora na upande mwingine wakasikilizwa. Hatuwezi kusikiliza shauri upande mmoja, kesi hii ina ina maslahi kwa umma kuna haja ya kuusikiliza na upande wa pili, nawapa siku saba muwasilishe utetezi na hati ya kiapo kinzani,” amesema Jaji Demelo.

Jaji Demelo alisema upande wa waleta maombi kama watakuwa na hoja za kujibu utetezi wawasilishe kabla ya Agosti 8, mwaka huu ambapo shauri hilo la madai litaanza kusikilizwa Agosti 6, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles