30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wamiliki wa viwanda watakiwa kutumia maonyesho ya Sabasaba kujitangaza

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara nchini wameshauriwa kutumia Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) kama uwanja wa kutangaza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyao.

Rai hiyo imetolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Julai 2, wakati akizindua maonyesho hayo katika viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam, katika maonyesho hayo yaliyobeba kauli mbiu isemayo ‘usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu’.

Mama Samia amesema maonyesho hayo ambayo yamejizolea umaarufu Afrika Mashariki na Kati hutembelewa na watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi hivyo yakitumika vizuri ni sehemu sahihi ya wafanyabiashara kupanua wigo wao kibiashara.

“Maonyesho ya biashara ni nyenzo muhimu ya kuwakutanisha wafanyabiashara na wanunuzi hivyo yakitumiwa vizuri huongeza tija katika sekta zinazolisha bidhaa kwa matumizi mbalimbali hususani za viwandani.

“Ninafahamu pia maonyesho haya yamejipatia umaarufu sana, nimepata faraja kufahamishwa kuwa maonyesho haya yamethibitishwa kuwa maonyesho makubwa na bora kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, niwapongeze TANTRADE na Wizara na muyakuze yawe makubwa zaidi,” amesema.

Katika hatua nyingine Mama Samia amewataka wakulima kulima mazao kwa wingi kwani Serikali inaendelea kujenga viwanda ambavyo malighafi yake itatoka hapa nchini hususani katika sekta ya kilimo.

“Serikali inaendelea kujenga viwanda na sehemu kubwa ya malighafi itatoka hapa nchini na hasa bidhaa zitokanazo na  kilimo hivyo wakulima watapaswa kuzalisha kwa wingi ili wawe na akiba nyingi kwa ajili ya chakula lakini pia kwa viwanda vyetu hapa nchini,” amesema Samia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles