22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

MAHAKAMA YAAMRU KIJANA ALIYENG’ANG’ANIA KWA WAZAZI AONDOKE

NEW YORK, Marekani


WAZAZI  wawili mjini New York nchini Marekani wamefanikiwa kushinda  kesi waliyokuwa wakipambana nayo ili kumuondoa kijana wao mwenye umri wa miaka 30 nyumbani kwao, baada ya kukaidi kuondoka

Kesi hiyo iliamriwa jana na Jaji wa Mahakama hiyo, Donald Greenwood na akamueleza  kijana huyo, Michael Rotondo, ombi lake la kutaka kuendelea kubaki nyumbani hapo kwa miezi sita zaidi haikubaliki

Katika mashtaka hayo ambayo waliyawakilisha wiki iliyopita, wazazi hao, Christina  na  Mark Rotondo walionesha nakala ya nyaraka walizokuwa wakimuamuru kuondoka nyumbani tangu Februari  2 mwaka huu na moja ya nakala ilikuwa ikimueleza kijana huyo kuwa kuna kazi zinapatikana hata kwa wenye historia ya tabia mbaya kama za kwake.

”Kuna kazi zinapatikana hata kwa wale wenye historia mbaya ya kufanya kazi kama wewe” ”Nenda katafute kazi-unapaswa kufanya kazi,”ilieleza moja ya nakala.

Mbali na nakala hizo, pia  wazazi hao waliiambia mahakama kuwa wampatia dola za Marekani 1,100 ili aondoke nyumbani na wakamtaka  auze baadhi ya vitu vyake ikiwemo gari yake mbovu aina ya Volkswagen Passat, lakini akakataa kuondoka.

Wakati wa kujitetea,  Rotondo ambaye alijiwakilisha mwenyewe mahakamani,  alisema kuwa mpaka sasa hafahamu ni kwa nini wazazi wake hawataki kusubiri kidogo ya kuondoka.

Alisema kuwa miezi sita ndio muda sahihi  kwa mtu ambaye alikuwa akiwategemea watu kuweza kujiandaa ili akaanze maisha mapya.

Jaji akiwa anatabasamu alimtaka kijana huyo azungumze na wazazi wake,na kuamua kwa hiyari kuondoka nyumbani, lakini Rotondo alikataa.

Kwa mujibu wa Kituo Cha Televisheni cha ABC, hata hivyo pamoja na utetezi wake huo, Jaji Greenwood  alimuwekea ngumu na kumuamru aondoke.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika shauri hilo,Rotondo alikiri kupokea kiasi hicho cha fedha na kukitumia na huku akikiri kutotoa msaada wowote katika familia na kisha akasema ataka rufaa kupinga hukumu  hiyo na amepanga kuondoka nyumbani hapo baada ya miezi mitatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,367FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles