30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

‘HAWA NDIYO WALIOKIDHI VIGEZO MAUDHUI KWA NJIA YA MTANDAO’

Norah Damian, Dar es Salaam

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imesema maombi 45 kati ya 262 yamekidhi vigezo na kupatiwa leseni kwa ajili ya utoaji huduma za maudhui kwa njia ya mtandao.

Akizungumza leo wakati wa kukabidhi leseni hizo, Mwanasheria wa TCRA, John Dafa, amesema maombi mengine 20 yamekidhi vigezo lakini wahusika bado hawajalipia ada kwa ajili ya kupatiwa leseni.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba, amesema gharama zilizowekwa zinalenga kuzuia uanzishwaji holela wa vyombo vya habari mtandaoni usiokidhi viwango vinavyotakiwa.

“Umiliki wa vyombo vya habari bila tozo unaweza kuleta utitiri wa vyombo hivi na ikawa changamoto katika usimamizi na kwa jamii pia,” amesema Kilaba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles