24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli: Watuhumiwa uhujumu uchumi kuweni makini na mnaowasikiliza

Anna Potinus, Dar es Salaam

Rais John Magufuli amewataka watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi walioagizwa kuwasilisha barua zao za kuomba msamaha katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuepukana na dhana ya kuwa msamaha huo ni wa uongo kwakuwa yeye ameutoa kwa dhati na kwamba hawezi kufanya hivyo kwa lengo la kuwatega.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Septemba 30, alipokuwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kusamehe watuhumiwa hao wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali.

“Hizi siku saba ni kwaajili ya wale ambao wamekwama inawezekana mwingine akawa amejifikiria zaidi katika siku ya leo hadi ya saba akatoa maamuzi yake ninafahamu wapo wanaodanganywa huu msamaha ni wa uongo,”

“Huwa hakuna msamaha wa uongo hauwezi ukatoa msamaha wa majaribio au wa kumtega mtu, msamaha ukishautoa ni msamaha la sivyo wewe uliyetoa utaibeba hiyo dhambi kwa Mungu, ninafahamu wapo wanaodanganywa na mawakili wao ili waendelee kuwachomoa pesa wanaawambia ukiomba msamaha maana yake unakuwa umeshajishtaki mwenyewe sasa hiyo ni shauri yao waamue wanamsikiliza nani,” amesema Magufuli.

Aidha ameitaka ofisi ya DPP kuharakisha juu ya suala hilo ili watuhumiwa hao waweze kutoka wakajumuike na familia zao kutokana na sababu kuwa waliingia kwa njia ya mahaka hivyo wanapaswa kutoka kwa njia ya mahakama hivyo wawafikishe kwenye vyombo vya sheria ili waweze kuachiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles