23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli aongeza siku saba watuhumiwa uhujumu uchumi kutubu

Anna Potinus

Rais John Magufuli ameongeza siku saba kwa watuhumiwa uhujumu uchumia ambao barua zao bado hazijafika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutokana na vikwazo mbalimbali ikiwemo kucheleweshwa kuandika barua kwenye magereza na barua nyingine kukwama kwenye ofisi za mikoa.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Septemba 30, alipokuwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kusamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali.

“Kama kweli wapo walikwamishwa na DPP umeniomba siku tatu mimi naona nikupe siku saba ili usije ukaniomba tena siku nyingine, nilitoa siku sita kwamba watuhumiwa wote wanaotaka kupata huu masamaha kwa kupitia taratibu za kisheria na wameitikia zaidi ya watu 467 na fedha Sh.  bilioni 107.842 zitaokolewa na nina uhakika hawatarudia makosa yao lakini nitoe tahadhari baada ya siku hizi saba kuisha wale wote watakaoshikwa kwenye makosa haya ya uhujumu uchumi sheria ichukue mkondo wake,”

“Nimetoa hizi siku saba na sitatoa nyingine lakini niwapongeze hawa 467 na mimi ningeomba ofisi ya DPP muharakishe ili watu waanze kutoka wakajumuike na familia zao kwasababu waliingia kwa njia ya mahaka watatoka kwa njia ya mahakama kwahiyo muwafikishe kwenye vyombo vya sheria ili waweze kuachiwa isije tena mtakapochambua mkakuta wamebaki 300,” amesema Magufuli.

Aidha amesema msamaha huo hautawahusu watuhumiwa wenye kesi mpya na kwamba wachukuliwe sheria kwakua msamaha huo ni kwa wale waliokwama tu.

“Watakaoshikwa na kesi za uhujumu uchumi leo, kesho na kuendelea wao waendelee na kesi zao za uhujumu uchumu maana huu msamaha hauwahusu hata kidogo kwani kuna wale ambao wana kesi mpya wao wapelekwe tu kwenye kesi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles