24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli: Madaraka yasiwagawe Watanzania

g1 (1)Na Bakari Kimwanga, Tanga

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli ameonya na kusema nafasi za madaraka zisiwagawe Watanzania.

Amesema kila mtu anawajibu wa kulitumikia taifa na watu wake bila kubaguliwa na wenye nafasi za uongozi.

Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jana kwa nyakati tofauti, alipokuwa akizungumza kwenye mikutano ya kampeni za kuomba kuchaguliwa katika wilaya za Muheza, na Pangani mkoani Tanga.

Alisema nchi inahitaji viongozi ambao hawatawagawa Watanzania kwa dini, kabila wala rangi zao.

“Nafasi zetu za madaraka zisitugawe Watanzania, wote tuna wajibu wa kulitumikia taifa na watu wake.

 

“Ninaomba nafasi ya urais si kwa ajili ya majaribio, kazi hii ninaiweza tena kwa vitendo, utumishi wangu serikalini katika kipindi cha miaka 20 kila mmoja anaujua,” alisema Dk. Magufuli

Akiwa njiani msafara wake,ulisimamishwa na wananchi wa Kijiji cha Mkata ambao waliwasilisha kero yao ya maji na kufungwa kwa kiwanda cha mbao cha Tuico.

Mmoja wa wakazi wa Mkata, Said Mkonje, alisema kufungwa kwa kiwanda hicho kumesababisha kukosekana ajira kwa vijana wengi wa eneo hilo.

Akijibu hoja  za wananchi hao Dk. Magufuli, aliwaomba wamwamini na atahakikisha kilio hicho kinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Katika hatua nyingine, CCM imejibu tuhuma zinazoelekezwa kwake za wizi wa kura kutoka kwa wapinzani.

Kauli hiyo, imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Mbowe kudai kuwa kukubalika kwa mgombea wa Chadema,Edward Lowassa, kazi iliyobaki ni kwa CCM kuiba kura.

Akijibu madai hayo jana jijini hapa, mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Abdallah Bulembo, alisema anashangazwa na madai hayo kutolewa na Chadema.

Alisema CCM haina mpango wa kuiba kura ila mgombea wao wa urais anakubalika na amekuwa akifanyakazi kusaka kura usiku na mchana kwa Watanzania.

“Leo ninapenda kumjibu Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema),  anadai eti CCM tunataka kuiba kura. Ninamjibu na kumwambia hatuna shida wala mpango huo.

“Mgombea wetu anakubalika hadi sasa tumefanya mikutano rasmi 48, isiyo rasmi 160 na mikoa 9, tumekuwa tukiamka saa 12 hadi saa 3 na tumekwenda katika zaidi ya majimbo 60,” alisema Bulembo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles