27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Slaa ajichanganya yupi anamlenga

ADAM MKWEPU NA VERONICA ROMWALD

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa amesema hana haja ya kuwazungumzia viongozi wanaomaliza muda wao madarakani, badala yake anamlenga kiongozi atakayekuwa rais wa nchi kwa miaka mitano ijayo.

Dk. Slaa alisema hayo Dar es Salaam jana katika mahojiano maalum na mwandishi mkongwe, Tido Mhando wa televisheni ya Azam.

Akijibu swali kuhusu kwa nini anamzungumzia tu  mgombea urais wa Chadema anayewakilisha Ukawa, Edward Lowassa badala ya kuzungumzia ufisadi kama mfumo mzima wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Slaa alisema:

“Tido, nilielezea juu ya   Serikali ya CCM akiwamo  Rais Kikwete (Jakaya) ndiyo iliyomlea Lowassa (Edward)… John Mnyika bungeni aliwahi kusema Kikwete ni dhaifu  hilo halina utata, lakini hivi sasa  hatumzungumzii Kikwete kwa kuwa anaondoka na ameshaagwa.

“Tunapoteza muda kwa mtu  ambaye kesho hayupo, hapa tunamzungumzia mtu ambaye tutakuwa naye  kama rais wetu kwa miaka mitano ijayo,”alisema Dk. Slaa.

Kuhusu kuwataja mafisadi wengine, katibu mkuu huyo wa zamani wa Chadema alisema hajawahi kupata kigugumizi cha kuwataja mafisadi na kudai kwamba aliwahi kuwataja baadhi ya viongozi  kwa ufisadi ndani ya ofisi ya Ikulu kwenye mikutano ya hadhara na hakukamatwa kwa kuwa alifanya utafiti.

“Nazungumzia hawa kwa kuwa madhara (impact) yao ni kubwa kuliko hao wengine lakini tutaendelea kuwapigia kelele kama ilivyo kwa watumishi wengine hadi wakaondolewa kwa hiyo tulikwenda kuwataja watu na sikumung’unya maneno,”alisema.

Katika mahojiano hayo maalum, Dk. Slaa alikiri kwamba alihama nyumbani kwake kwa muda kutokana na vitisho dhidi yake na kudai kuwa alitoa taarifa ya kupatiwa ulinzi   kuhakikisha usalama wake.

“Ni kweli na ndiyo maana sikuficha kama nilikuwa Serena hata hivyo sikuona kuwa ni kitu cha ajabu na mbona watu hawajiulizi kwamba 2010 kipindi nagombea urais nililala Serena kwa nini leo liwe jambo la ajabu wakati hii si mara yangu ya kwanza,”alisema Dk. Slaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles