27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Magufuli kuanza ziara leo Arusha

Tanzania's President elect Magufuli addresses members of the ruling CCM at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es SalaamABRAHAM GWANDU NA JANETH MUSHI, ARUSHA

RAIS Dk. John Magufuli, leo anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, alisema kuwa Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili leo saa nane mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Kutokana na ziara hiyo, Ntibenda aliwaomba wananchi na wakazi wa Jiji la Arusha kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Magufuli.

Ziara hiyo ni ya kwanza kufanywa na rais katika Mkoa wa Arusha tangu achaguliwe katika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana.

Hata hivyo, mkuu huyo wa mkoa hakuweka wazi shughuli atakazofanya Rais Magufuli mkoani hapa, lakini chanzo chetu cha habari kilisema kwamba anatarajiwa kutoa nishani  kwa maofisa wa jeshi katika Chuo cha Jeshi cha Monduli siku ya Jumamosi.

Pamoja na hilo, pia atafanya ziara za kushtukiza katika taasisi na mashirika ya umma ikiwamo ofisi za Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).

Mbali na Tanapa, huenda akatembelea pia ofisi za AICC, Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) na Mahakama ya Afrika na baadhi ya ofisi za halmashauri za wilaya za jirani na Jiji la Arusha.

Kutokana na ziara hiyo ya kwanza ya Rais Magufuli mkoani hapa, kumekuwa na pilikapilika za maandalizi ya kumpokea ikiwamo ukarabati wa Ikulu ndogo iliyoko barabara ya Mahakama Kuu ambako inaelezwa ndipo atakapofikia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles