22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mama aua watoto wake kwa sumu

Philip KalangiNA SHOMARI BINDA, MUSOMA

MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jila la Elizabeth Mugendi (24), mkazi wa Kijiji cha Kamugesi, Tarafa ya Makongoro, Wilaya ya Butiama mkoani Mara, amewaua watoto wake wawili kwa kuwanywesha sumu kutokana na ugomvi na ndugu yake.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Musoma jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philip Kalangi, alisema tukio hilo lilitokea Januari 16, mwaka huu katika kijiji hicho ambapo watoto hao walifariki dunia walipofikishwa hospitali.
Alisema mama huyo baada ya kuwanywesha sumu watoto wake hao, Nicolaus Mauma (4) na Wanzagi Katoki (2) naye alikunywa sumu kwa lengo la kujiua.

Kamanda Kalangi alisema kutokana na maelezo ya mwanamke huyo ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Butiama baada ya kuwanywesha sumu watoto wake, alichukua uamuzi huo kutokana na kunyanyaswa na ndugu yake.

Alisema mwanamke huyo kutokana na maelezo yake, alidai ndugu yake aliyemtaja kwa jina la Warioba Mugendi, amekuwa na tabia za kumpiga kila wakati na uamuzi aliochukua alitaka kuondoka duniani yeye na watoto wake ili ajiepushe na manyanyaso.
Kamanda Kalangi alisema kabla ya tukio hilo, ndugu yake huyo alimpiga sehemu mbalimbali za mwili wake kutokana na kuangusha glasi.
“Mwanamke huyu amewanywesha sumu watoto wake inayodaiwa ni ya kuulia wadudu na yeye mwenyewe kunywa kutokana na kile alichodai ugomvi aliokuwa nao yeye na ndugu yake.
“Tulipata taarifa hizi na kuzifuatilia ambapo baada ya kufikishwa hospitalini watoto walifariki dunia wakiwa wanapatiwa matibabu na mama yao bado anaendelea kupata matibabu akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi,” alisema Kalangi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles