Magufuli awaapisha mabalozi wapya watano

0
864
Mabalozi wakila kiapo

Anna Potinus

Rais John Magufuli leo Jumamosi Novemba 23, amewaapisha mabalozi wateule watano watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.

Akizungumza baada ya kuapisha mabalozi hao katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, Rais Magufuli amewatakia kheri na katika majukumu yao ya kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa na kuwataka kuripoti katika vituo yao vya kazi katika kipindi kisichozidi wiki moja.

Mabalozi hao ni Maj. Gen Shigongo ambaye amekuwa Balozi wa Tanzania Nchini Misri, Mohamed Mtonga aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Abu Dhabi (UAE), Jestas Abouk Nyamanga aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji.

Wengine ni Ali Mwadini alitechaguliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Saud Arabia na Dk. Jilly Maleko aliyechaguliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Burundi.

Kwa upande wake Waziri Mkuu, Kassim majaliwa amewataka mabalozi hao na mabalozi wengine wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kusimamia vizuri fedha na mali zilizopo katika balozi hizo.

Aidha amewataka kusimamia vizuri utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ili Tanzania inufaike na uhusiano mzuri uliopo kati yake na nchi wananzoziwakilisha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here