30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kijana wa miaka 19 jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka 10

Malima Lubasha, Serengeti

 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Serengeti mkoani Mara, imemuhukumu mkazi wa Kijiji cha Parknyigoti, Machaba Makoro (19) kifungo cha maisha jela baada ya kukiri kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 10 mwanafunzi wa Shule ya Msingi Parknyigoti.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Renatus Zakeo, akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Adelina Mzalifu, alidai tukio hilo lilitokea Novemba 20 mwaka huu majira ya jioni na kwamba Makoro ni mkazi wa kitongoji cha Manchira Kijiji cha Parknyigoti.

Alisema mshtakiwa huyo ambaye anaishi jirani na mtoto huyo, alifika eneo ambalo mtoto huyo alikuwa anacheza na wenzake na kumchukua akampeleka kwa nyumbani kwa bibi yake kisha kumbaka na kumsababishia majeraha sehemu za siri.

Zakeo alisema mama mzazi wa mtoto huyo, Monica Mathias, alipotoka shambani  jioni alikuta mtoto huyo anatokwa na damu ambapo wenzake walimweleza kwamba Machaba ndiye alimchukuwa na kwenda kumfanyia kitendo hicho kwa bibi yake.

Alidai Monica alitoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho Jacob Mbota na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha Kituo cha Polisi cha Mugumu hatimaye kufikishwa mahakamani.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa alikiri kufanya kitendo hicho, ambapo Hakimu Mzalifu, alimuhukumu kutumikia kifungo cha maisha jela.

Hakimu Mzalifu alisema mshtakiwa hakuisumbua mahakama na kuilahishia kutoa uamzi bila shaka yoyote hivyo anamuhukumu kwenda jela maisha kwani vitendo vya kuwadhalilisha watoto vimekuwa vikiongezeka katika jamii.               

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles