23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

RC Kagera awatia ndani walimu, mkandarasi kwa kushindwa kusimamia mradi wa ujenzi

Nyemo Malecela -Kagera

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amewaweka rumande watumishi wanne na mkandarasi mmoja kwa kushindwa kusimamia mradi ya ukarabati wa shule kongwe za Bukoba Sekondari na Kahororo zilizoko Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Waliowekwa ndani ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kahororo, Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bukoba, Mhandisi wa Manispaa ya Bukoba, Ofisa Manunuzi wa Manispaa ya Bukoba na Mhandisi wa kampuni inayojenga miradi hiyo, David Michael.

Gaguti alimwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, kuwaweka ndani wasimamizi hao jana (juzi) alipotembelea shule hizo za Sekondari ya Rugambwa na Kagemu ambazo zinaendelea kukarabatiwa.

Miradi hiyo ya ukarabati ya shule kongwe za Kahororo, Rugambwa, Kagemu na Bukoba, unagharimu Sh bilioni 2,595,890,485.33 zilizotolewa na Serikali ili majengo ya shule hizo zirejee katika hali nzuri.

Licha ya fedha kuingizwa katika kila akaunti ya shule husika, ukarabati umechukua muda mrefu kukamilika au kuendelea kusuasua.

Katika Shule ya Sekondari Kahororo hakuridhishwa na ukarabati unaoendelea chini ya kampuni ya Mzinga Holding Company na kumweleza Malimi kuwaweka chini ya ulinzi Mkuu wa Shule hiyo, Marck Ogambage kwa uzembe wa kushindwa kumsimamia Mhandisi Festo Tarimo na Ofisa Manunuzi wa Manispaa ya Bukoba, Batreth Rwiguza kwa kufanya uzembe wa mchakato wa manunuzi ya vifaa vya ujenzi.

Wengine waliowekwa ndani ni Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Bukoba, George Geofrey kwa kutosimamia ipasavyo ukarabati na Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bukoba, Siasa Focus.

Shule ya Sekondari Kagemu ilipewa Sh milioni 152,000,000 na tayari muda wa ukarabati umeisha na zimelipwa milioni 49,485,277.22 wakati Shule ya Sekondari Kahororo ilipewa Sh milioni 893,883,994 kati ya hizo zimetumika  Sh milioni 297,966,594.96 na muda wa ukarabati umeisha bila kazi kukamilika. 

Shule ya Sekondari Rugambwa ilipewa Sh milioni 872,800,297 na zilizotumika ni Sh milioni 275,125,889.25 ambapo muda wa ukarabati umeisha.

Kwa upande wa mradi wa barabara ya urefu wa kilometa 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles