29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Magufuli atoa msamaha kwa wafungwa 5,533

Anna Potinus

Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 5,533 waliofungwa kati ya siku moja na mwaka mmoja na wale waliofungwa kwa miaka mingi na tayari wametumikia sehemu kubwa ya vifungo vyao na kubakisha kipindi kisichozidi mwaka mmoja.

Rais Magufuli ametoa msamaha huo leo Jumatatu Desemba 9, alipokuwa kizungumza katika maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya uhuru wa Tanzania bara yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.

“Baadhi yenu mtakumbuka miezi michache iliyopita nilitembelea baadhi ya magereza ikiwemo gereza ma Butimba ambapo nilishuhudia kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa wafungwa na kwa taarifa niliyopewa hali kama hiyo haiku kwenye gereza hilo tu bali ni kwa magereza yote nchini na mpaka leo tuna wafungwa 17,547 na mahabusu 18,256 hivyo kwa pamoja wanakuwa 35,803 hii ni idadi kubwa.

“Baadhi ya wafungwa wamefungwa kwa makosa madogo madogo kama kuiba kuku, kumtukana rafiki yake, kujibizana na mpenzi wake au mshikaji wake na wengine kwa kukosa mawakili wa kuwatetea vizuri katika kesi zao lakini wengine kwa kushindw akulipa fani na kuna wengine wamefungwa kwa kuonewa.

“Kama binadamu hali niliyojionea pale Butimba ilinihuzunisha na kunisikitisha sana ilikuwa hali mbaya hivyo kwa kutambua kuwa hakuna mwanadamu aliyemkamilifu na wote hapa tumeshatubu na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na kwa kutambua wafungwa wengi wanajutia makosa yao na hawako tayari kuyarudia ninapenda nitumie kwa mujibu wa madaraka niliyopewa ya kusamehe au kufuta adhamu ya mtu aliyetiwa hatiani na mahakama nimeguswa na nimeamua kusamehe jumla ya wafungwa 5,533,” amesema Rais Magufuli.

Aidha ameagiza wafungwa hao Ni matumaini kuachiwa mara moja bila kucheleweshwa wala kuwawekea mizengwe kwani orodha ya majina yao yote anayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles