25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Mbowe, Lowassa wampa tano Magufuli

Anna Potinus

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Waziri Mkuu Msaafu, Edward Lowassa wamempongeza Rais John Magufuli kutokana na juhudi mbalimbali ananzifanya katika kuliongoza taifa.

Akizungumza katika maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya uhuru wa Tanzania bara yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza, Mbowe amesema kuna ulazima wa kuwepo maridhiano na mshikamano ili taifa lizidi kusonga mbele.

“Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya uhuru kama udhibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, upendo na mshikamano katika taifa letu, ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia ili tujenge taifa lenye upendo na mshikamano.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe

“Mheshimiwa rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika taifa kwani kuna wengine wanalalamika na kuumia basi utumie nafasi hii kuliweka taifa katika nafasi ya utengamano,” amesema Mbowe.

Kwa upande wake Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kutumia amani kama msingi wa kuleta mshikamano wa nchi na kuwasishi Watanzania kuendelea kumuunga mkono katika kuleta mabadiliko nchini.

“Kama Rais Magufuli ataachiwa akamaliza miaka yake 10 nchi hii itabadilika itakuwa kubwa na yenye maendeleo makubwa sana kwa hiyo ninaomba tumuunge mkono tumsaidie ili nchi yetu izidi kwenda mbele,” amesema Lowassa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles