26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

MAGARI 15,000 YASIYOLIPIWA KODI YANASWA

Na MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Udalali ya Yono Auction Mart imefanikiwa kukamata magari 15,000 yasiyolipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart, Scholastica Kevela, alipozungumza wakati wa operesheni ya kukamata magari na wafanyabiashara wasiolipa kodi.

Kevela alisema magari hayo ni yale yaliyokamatwa kuanzia Januari hadi Mei, mwaka huu na tayari baadhi ya wamiliki wamefanikiwa kuyakomboa kwa kulipa kodi na magari 300 bado wanayashikilia.

Alisema magari yote yaliyokamatwa ni ya wadaiwa sugu wa kodi mbalimbali za TRA na kueleza kuwa, iwapo hawatayakomboa watasubiri maelekezo kama yauzwe ili kukombia deni wanalodaiwa wenye magari.

Pia alisema wamefanikiwa kukamata shehena ya mali mbalimbali za wafanyabiashara wasiotoa Risiti za Kielektroniki (EFDs) pindi wanapofanya mauzo, jambo ambalo ni kosa kisheria.

“Yono tunafanya kazi ya kukusanya kila aina ya kodi ambayo baadhi ya wafanyabiashara wanaikwepa, mmeona vitu kama viti, matairi, makopo ya rangi na vitenge, yaani yadi imejaa, tumekamata hivi kwa wengine kushindwa kutumia mashine za kielektroniki,” alisema.

Kevela alisema Watanzania wanapaswa kuhakikisha kila wanaponunua wanaomba risiti na wafanyabiashara wahakikishe wanatoa risiti kwa kila bidhaa wanayouza ili kukwepa usumbufu.

“Nawasihi Watanzania walipe kodi bila shuruti, kwa sababu itaonekana kama unyanyasaji, lakini ukweli ni kwamba kila mtu anapaswa kulipa kodi, kama unafanya biashara hakikisha unalipa kodi tena kwa EFDs,” alisema.

TRA imeipa Yono zabuni ya kukusanya madeni yake ya kodi kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Njombe, Mbeya, Iringa na Zanzibar na hadi sasa imefanikiwa kukamata mali nyingi za wadaiwa sugu

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles